Pata taarifa kuu
MYANMAR

Aung Sun Suu Kyi ateuliwa tena kuongoza upinzani nchini Myanmar

Kiongozi wa upinzani nchini Myanmar Aung San Suu Kyii ameteuliwa kwa mara nyingine tena kuwa kiongozi mkuu wa upinzani katika mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wanachama wa National League for Democracy NLD uliofanyika jumapili hii mjini Yangon.

AFP PHOTO / JUNG YEON-JE
Matangazo ya kibiashara

Baada ya uamuzi huo kupitishwa Suu Kyi amewashukuru wanachama kwa ushirikiano wao wa miaka ishirini na tano ya NLD na pia ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wanachama wapya.

Uamuzi wa kuteuliw akwa mara nyingine tena kwa Suu Kyi umebezwa na baadhi ya wanachama ambao walitarajia kuona damu changa za vijana zikishika nyadhifa za juu katika muungano wa wapinzani hususani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Suu Kyi mwenye umri wa miaka sitini na saba amewahi kukabiliwa na kifungo cha ndani kwa mia ishirini kutokana na kuwa mstari wa mbele kukosoa utawala wa kijeshi na pia amewahi kujitwalia tuzo ya amani ya Nobel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.