Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Mahakama Kuu ya Pakistan imeamuru Waziri Mkuu akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa

Mahakama Kuu nchini Pakistan imeamuru kukamatwa na kufikishwa makamani kwa waziri mkuu kutokana na kujihusisha na mikataba ya kifisadi wakati akiwa waziri ndani ya baraza la mawaziri la nchi hiyo. Mahakama hiyo imetoa amri ya kukamatwa kwa waziri mkuu Raja Pervez Ashraf na kumhusisha kesi ya rushwa wakati akiwa waziri wa maji na nishati na kutumia madaraka yake vibaya.

Reuters / Stringer
Matangazo ya kibiashara

Ashraf akiwa na wadhifa huo inadaiwa na mahakama hiyo kuwa aliingia mikataba mibovu ya manunuzi ya mitambo ya kufua umeme katika moja ya miradi nchini humo na hivyo kuisababishia hasara serikali.

Kufuatia tuhuma hizo waziri mkuu Ashraf anaonekana kuvunja miiko ya uongozi kwa kuvunja misingi ya uwazi na kujiingiza katika vitendo vya udanganyifu ili kujipatia fedha kinyume na taratibu na maadili ya kazi.
 

Mahakama hiyo imeagiza kukamatwa pia kwa maafisa wengine 16 wakijumuishwa na waziri mkuu huyo mkuu wa Pakistan kuhusiaana na tuhuma hizo za rushwa na kutumia madaraka vibaya.

Mahakama kuu ya Pakistan imeagiza mamlaka za serikali zinazohusika kumfikisha mahakamani waziri mkuu Ashraf siku ya Alhamisi ya wiki hii ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.