Pata taarifa kuu
Pakistan-Uingereza

Hali ya mwanaharakati aliepigwa risase nchini Pakistani ni ya kuridhisha

Binti mwenye umri wa miaka 14 mwanaharakati, Raia wa Pakistani aliyepigwa risasi na kundi la wanamgambo wa Taliban ameelezwa kuwa hali yake ya kiafya inaridhisha.Malala Yousafzai alifika nchini Uingereza jana baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Birmingham kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Queen Elizabeth mjini humo.

Malala Yousufzai, akipelekwa hospitalini
Malala Yousufzai, akipelekwa hospitalini ©Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Mganga mkuu wa Hospitali hiyo, David Rossi ameeleza matumaini yao juu ya Hali ya Malala.

Malala alipigwa risasi na Taliban wakati akirejea nyumbani toka shuleni kwenye bonde la Swat ambalo awali lilikuwa likidhibitiwa na kundi la wanamgambo wa Taliban, ikiwa ni adhabu kwa kile kilichoelezwa kushiriki kwake binti huyo katika kampeni za kuhamasisha maswala ya haki ya elimu kwa mtoto wa kike.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.