Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Watu wenye silaha washambulia basi na kuua watu 18 huko Pakistan

Watu wenye silaha wameshambulia basi moja katika eneo la Kaskazini mwa nchi ya Pakistan na kuuwa waumini kumi na wanane wa dhehebu la Washia waliokuwa wanasafiri kwa kutumia basi hilo.

Eneo ambalo shambulizi la basi limefanywa na watu wenye silaha na kuua abiria 18
Eneo ambalo shambulizi la basi limefanywa na watu wenye silaha na kuua abiria 18
Matangazo ya kibiashara

Basi hilo lilisimamishwa kabla ya abiria hawajaamrishwa kushuka katika Wilaya ya Kohistan wakati basi hilo linafanya safari yake ya kutoka katika Jiji la Rawalpindi kuelekea Gilgit kwenye makao makuu ya Jeshi.

Mkuu wa Polisi katika eneo hilo Mohammad Ilyas amethibitisha watu wenye silaha kufanya shambulizi hilo na watu kumi na wanane kupoteza maisha huku wengine wanane wakijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Eneo ambalo linatajwa kutokea kwa shambulizi hilo lililolenga basi la abiria lipo jirani na ngome ya Kundi la Wanamgambo wa Taliban linalotambulika kama Bonde la Swat.

Manusura wa tukio hilo wamesema kuwa watu wenye silaha kati ya saba au nane ndiyo ambao walitekea basi hilo na kushinikiza lisimame kisha kuwaamuru abiria wote kutoka kwenye gari hilo kabla ya kuwashambulia.

Shambulizi hilo limetokea jirani na Mji wa Harban uliopo kilemeta mia mbili na nane Kaskazini mwa Mji Mkuu Islamanad na hakuna Kundi lolote ambalo limethibitisha kutekeleza tukio hilo.

Wengi wamehusianisha tukio hilo kama kulipiza kisasi kulikofanywa na Wasunni ambao walishuhudia watu wawili kutoka madhehebu hayo wakiuawa sikua kadhaa zilizopita katika Jiji la Gilgiti mauaji ambayo yanahusishwa kufanywa na Washiha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.