Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Mahakama kuu nchini Pakistan yathibitisha mashtaka dhidi ya Waziri Mkuu Yousuf Raza Gilan

Mahaka ya juu nchini Pakistan imemuagiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo Yousuf Raza Gilani kutokea mahakamani hapo tarehe 13 mwezi huu kujibu mashtaka ya kwanini alikataa kufungua kesi za rushwa zinazowakabili viongozi katika serikali.

Waziri Mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gilani
Waziri Mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gilani Reuters/Mian Khursheed
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa mahakama ambao umetolewa hii leo, umekuja kufuatia awali wakili anayemtetea Waziri Mkuu Gilan kuwasilisha pingamizi mahakamani hapo kupinga mteja wake kushtakiwa kwa makosa ya kukiuka katiba ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Islamabad, wakili wa Waziri Mkuu Gilani, Aitzaz Ahsan amedhibitisha kupokea amri ya mahakama inayomtaka yeye na Waziri Mkuu Gilani kufika mahakamani tarehe 13 ya mwezi huu kwaajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Mapema hii leo jaji anayesimamia kesi hiyo aliwaambia majaji wa mahakama kuu kuwa tayari wamekusanya ushahidi wa kutosha ambao unamuhusisha moja kwa moja Waziri Mkuu Gilani kwa kushindwa kufungua kesi dhidi rais Asif Ali Zardari pamoja na viongozi wengine wa serikali wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa.

Nae jaji wa mahakama kuu Nasir-ul-Mulk amesema kuwa baada ya kusikiliza upande wa mashtaka mahakama yake imeridhishwa na ushahidi uliopo na kwamba ni lazima Waziri Mkuu Gilani apande kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa hatua hiyo ya mahakama kufufua upya mashtaka hayo yanalenga kuidhoofisha serikali na kutengeneza mazingira ya kutaka kufanyike uchaguzi mkuu mwingine endapo Waziri Mkuu Gilani atapatikana na hatia.

Tarehe 19 ya mwezi wa kwanza Waziri Mkuu Gilani alipandishwa katika mahakama kuu ya nchi hiyo ambapo alitetea uamuzi wake wakutofungua kesi hizo akidai kuwa rais analindwa na katiba ya nchi na asingeweza kumfungulia mashtaka.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.