Pata taarifa kuu

Aliyekua waziri wa Pakistan, Imran Khan aachiliwa kwa dhamana

Nairobi – Mahakama ya Juu ya Pakistan mapema leo imeamuru kuachiliwa kwa dhamana kwa aliyekua waziri wa Pakistan Imran Khan ,kwa kile mahakama hiyo inasema kuwa  kitendo hicho sio sawa na ni kinyume na sheria.

Polisi wamsindikiza mahakamani aliyekua Waziri wa Pakistan Imran Khan
Polisi wamsindikiza mahakamani aliyekua Waziri wa Pakistan Imran Khan AFP - AAMIR QURESHI
Matangazo ya kibiashara

Kitendo cha kukamatwa kwake mapema wiki hii, kilisababisha kuzuka kwa ghasia za wenyewe kwa wenyewe nchini Pakistan. Jaji Mkuu wa Pakistan, Umar Ata Bandial amemwambia Khan kwamba kukamatwa kwake ni batili, hivyo mchakato mzima unahitaji kuangaliwa upya.Khan anashtumiwa kwa madai ya ufisadi.

Kulingana na wakili wake Khan, Faisal Chaudhry mahakama imempa Khan dhamana ya wiki mbili.Jopo la majaji watatu limeombwa kusikiliza ombi la Khan katika mahakama ya Islamabad kupinga kukamatwa kwake kwa madai ya ufisadi.

Vilevile mahakama hiyo imemtaka waziri huyo mkuu wa zamani kushirikiana na Ofisi ya Kitaifa ya Uwajibikaji, ambayo inachunguza mashtaka dhidi yake.

Baada ya uamuzi huo wafuasi wake Khan walionekana wakisherehekea.

Kukamatwa kwa Khan siku ya jumanne kunakuja baada ya miezi kadhaa ya mzozo wa kisiasa na baada ya jeshi lenye nguvu kumkemea Khan, kutokana na madai kuwa ofisa mmoja mkuu meja jenerali, Faisal Naseer, alihusika katika njama ya kumuua, katika kipindi ambacho alipigwa risasi mguuni mwaka jana.

Karipio hilo la Jumatatu jioni lilisisitiza jinsi uhusiano wa Khan ulivyozorota na jeshi lenye nguvu, ambalo liliunga mkono kuibuka kwake madarakani mnamo 2018 lakini liliondoa uungwaji mkono wake kabla ya kura ya bunge ya kutokuwa na imani iliyomuondoa madarakani mwaka jana.

Taarifa kutoka idara ya mahusiano ya umma ya jeshi, imeyakashfu madai hayo, ikisema ni ya kubuni na yenye nia mbaya.Kufikia sasa karibia watu 2000 wanashikiliwa na polisi kwa kusababisha vurugu tangu kukamatwa kwa Khan siku ya jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.