Pata taarifa kuu
MAREKANI-JOE BIDEN

Biden atangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa mapinduzi Myanmar

Rais wa Marekani Joe Biden ameidhinisha sheria ya kiutendaji ya kuweka vikwazo vipya dhidi ya viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Burma na kuwataka kurejesha demokrasia nchini humo. 

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kwenye sheria hiyo Biden amewataka viongozi wa mapinduzi kumuachilia huru kiongozi wa chama cha NLD Aung San Suu Kyi na wenzake wanaoshikiliwa kusikojulikana tangu jaribio la mapinduzi.

 

Biden amesema sheria hiyo itawezesha utawala wake "kuwawekea vikwazo haraka ambao walihusika na mapinduzi, maslahi yao ya kibiashara sambamba na jamaa zao wa karibu". Rais Biden ameongeza kuwa wiki hii Marekani itabainisha awamu ya kwanza ya wale wataoguswa na vikwazo hivyo na vilevile inawazuia majenerali nchini Burma kuweza kuzifikia mali zenye thamani ya dola bilioni 1 katika fedha za serikali ya Burma zilizoko nchini Marekani.

 

Amesema utawala wake utabainisha awamu ya kwanza ya malengo ya vikwazo wiki hii, ingawa viongozi wengine wa jeshi la Myanmar tayari wameorodheshwa kutokana na ukatili dhidi ya Waislamu wa Rohingya

 

Mapinduzi ya kijeshi ya Februari mosi ambayo yalimuondoa mamlakani kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia Aung San Suu Kyi, yalitokea chini ya wiki mbili baada ya Biden kuapishwa na kuonekana kuwa mtihani wa mapema kwa kiongozi katika kushughulikia migogoro ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.