Pata taarifa kuu
CHINA-WHO

Coronavirus: Timu ya WHO kutoa ripoti kuhusu uchunguzi wake Wuhan

Wataalam kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) wanaohusika na kuchunguza asili ya janga la Corona wanaandaa mkutano na waandishi wa habari leo Jumanne, baada ya karibu mwezi mmoja wa mazungumzo mamlaka nchini China.

Nembo ya shirika la afya duniani, WHO
Nembo ya shirika la afya duniani, WHO Fabrice Ciffrini / AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Wataalam kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) wamekuwa katika ziara ya kikazi katika mji wa Wuhan nchini China, eneo linalodaiwa kuwa chimbuko la virusi vya Corona.

WHO imebaini kwamba mkutano huo na waandishi wa habari utafanyika saa 07:30 saa za kimataifa, na kwamba wataalam wa China waliohusika katika uchunguzi pia watakuwepo.

Walipowasili katika mji wa Wuhan Januari 14, wataalam hao wa WHO kwanza waliwekwa karantini kwa wiki mbili, kama tahadhari ya kiafya, kabla ya kuanza kazi yake, ikitembelea soko la jiji hilo ambalo visa vya kwanza vya maambukizi viliripotiwa, na vile vile Taasisi ya Virolojia inayohusika na utafiti wa janga hili.

Hivi karibuni mkuu wa kitengo cha dharura wa WHO Mike Ryan, alisema kuwa shirika hilo limetafuta uthibiti wa matarajio na kusema hakuna hakikisho la majibu kwa sasa. Mmoja wa wataalamu wa ujumbe huo wa WHO Thea Fischer, pia aliliambia shirika la habari la REUTERS kwamba ni muhimu kukumbuka kuwa mafanikio ya kundi hilo na kufuatilia asili ya virusi hivyo vinategemea kikamilifu uwezo wa kufikia vyanzo husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.