Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yavunja ukimya kuhusu nia yake kushiriki mazungumzo

Nchi ya Korea Kaskazini imevunja ukimya kuhusu kutaka kuwa na mazungumzo na nchi ya Marekani na maridhiani na nchi ya Korea Kusini, ikisema inataka kuwa na eneo lenye amani, ikikanusha madai kuwa vikwazo ndivyo vilivyoshinikiza nchi hiyo kuja kwenye meza ya mazungumzo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un. 路透社
Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa kwenye kituo cha taifa cha KCNA imekuja wakati huu mazungumzo ya maridhiano kati yake na Korea Kusini yakiendelea baada ya miezi kadhaa ya sintofahamu kwenye eneo la rasi ya Korea kuhusu mpango wake wa Nyuklia.

Awali ukimya wa nchi ya Korea Kaskazini ulizusha hofu kuhusu nia yake ya kurejea kwenye mazungumzo hata baada ya kuripotiwa kuandaliwa mkutano wa ana kwa ana kati ya rais Donald Trump na Kim Jong-Un pamoja na mwenzake wa Korea Kusini.

Taarifa ya Korea Kaskazini licha ya kutozungumzia moja kwa moja mkutano wa viongozi hao, imesema tu kuna uwanda mzuri wa mazungumzi yenye tija kati yake na Korea Kusini yaliyopelekea kuandwaliwa kwa mazungumzo na Marekani.

Pyongyang inasema msomamo wake unatokana na nguvu iliyonayo na sio udhaifu licha ya kuwa inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Taarifa hiyo imekashifu utawala wa Washington, Seoul na Tokyo kwa kuhoji utayari wake wa kushiriki kwenye mazungumzo na nia yake ya kutaka kuachana na mpango wa nyuklia.

Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in amesema mwezi ujao anatarajia kukutana na Kim Jong-Un na kuongeza kuwa kuna uwezekano ukawa ni mkutano pia utakahusisha viongozi watatu akiwemo rais wa Marekani Donald Trump.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za awali Jae-in ataanza kukutana na Kim Jong-un mwezi ujao kwaajili ya mazungumzo kabla ya kuandaliwa kwa mkutano rasmi wa kwanza wa ana kwa ana kati ya rais Trump na utawala wa Pyongyang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.