Pata taarifa kuu
PAKISTAN-MAREKANI

Wapiganaji wa Taliban wafanya shambulio kwenye kambi ya jeshi la Pakistan na kuua wanajeshi 8

Askari nane wa jeshi la Pakistan wamedhibitishwa kuuawa kufuatia shambulizi la kushtukiza lililofanywa na wapiganaji wa kundi la Taliban kwenye kambi moja ya polisi mjini Kurram.

Moja ya mashambulizi ambayo yamefanywa na wapiganaji wa Taliban nchini Pakistan hivi karibuni
Moja ya mashambulizi ambayo yamefanywa na wapiganaji wa Taliban nchini Pakistan hivi karibuni AFP/Photo
Matangazo ya kibiashara

Polisi kwenye mji huo wamesema kuwa wapiganaji hao walifanya shambulio la kushtukiza wakati wanajeshi wakiwa kwenye mapumziko yao ya kawaida na kuwaua askari 8 na kujeruhi wengine zaidi ya 15.

Eneo ambalo wapiganaji hao wametekeleza uvamizi huo ndilo eneo ambalo jeshi la pakistan lilifanikiwa kulichukua chini ya himaya ya kundi la Taliban kwenye mji wa Jogi.

Mji wa Jogi ndio umekuwa ngome kubwa ya wapiganaji wa Taliban kutekeleza mashambulizi yao na ndilo eneo ambalo kiongozi wa kundi hilo nchini Pakistan Hakimullah Mehsud alizaliwa.

Katika hatua nyingine rais wa Marekani Barack Obama kwa mara ya kwanza amekiri nchi yake kuhusika na mashambulizi ya anga yanayofanywa na ndege zisizo na rubani kwenye maeneo ya Pakistan.

Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Marekani kukiri kuhusika na mashambulizi hayo ya anga katika nchi ya pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.