Pata taarifa kuu

Marekani yaitaka Pakistan kuchukuw ahatuwa za kuangusha ngome za wanamgambo walioko Afghanistani

Marekani imeitaka Pakistan kuchukuwa hatua za kuangusha ngome za wanamgambo walioko nchini Afghanistan wanaoungwa mkono na baadhi ya watu katika serikali ya Pakistan na kuhamasisha makundi ya Taliban kufanya mazungumzo ili kumaliza mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka kumi nchini humo.

Helikopta mpakani wa Pakistani na Afghanistani
Helikopta mpakani wa Pakistani na Afghanistani REUTERS/Nikola Solic
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa marekani, Hillary Clinton ameahidi kuwa Marekani itasaidia zaidi katika kufanikisha mapambano dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Afghanistan wanaotumia ardhi ya Pakistan kushambulia marekani, lakini haikiwekwa bayana ni namna gani marekani itashiriki.

Mwana diplomasia huyo ameitumia siku ya leo kwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Pakistan baada ya kumaliza mazungumzo ya saa nne nchini Afghanistan hapo jana, mazungumzo yaliyolenga kumalizika haraka kwa vita vya muda mrefu vilivyopiganwa na marekani.

Mahusiano kati ya Pakistani na marekani yaliyumba baada ya vikosi maalum vya marekani kuvamia Pakistani na kumuua kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden, na shutuma za marekani dhidi ya Pakistani juu ya shambulio la ubalozi wa marekani mjini Kabul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.