Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Pakistan yajitetea kuhusu kuuliwa kwa Osama Bin Laden katika ardhi yake

Serikali ya Pakistan imesema Maafisa wa Ujasusi duniani wanastahili kulaumiwa kuwa kushindwa kubaini aliyekuwa Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliyeuawa na Majeshi ya Marekani alikuwa anaishi nchini mwao.

Magazeti ya nchini Pakistani
Magazeti ya nchini Pakistani REUTERS/Mohsin Raza
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani ametoa kauli hiyo na kuilaumu Marekani kwa kusema hakuna sababu ya kulilaumia taifa lake licha ya kubebeshwa lawama za Osama kuishi jirani na Kambi yao ya Jeshi.
Kiongozi wa Shirika la Kujasusi la Marekani CIA Leon Panetta ameahidi kutolewa kwa picha za mwili wa Osama hadharani huku akisifia mbinu zao za kiintelijensia ndiyo zaimefanikisha kifo cha Kiongozi huyo wa Al Qaeda.

Mkuu wa CIA
00:23

LEONEL PANETA MKUU WA CIA 04MAY2011

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru eneo lililoshambuliwa mwaka 2001 la Zero Square kesho huku Mwenyekiti wa Usalama wa Ndani wa Marekani, Peter King amesema taarifa za washirika wa zamani wa Al Qaeda zilisaidia mpango wao.

Nao wachambuzi wa mambo wanasema lawama zinazorushwa kwa Pakistan na mataifa mengine ni lazima zifikie kikomo na kuanza kuweka mikakati mipya ya kupambana na ugaidi kama anavyoeleza Mchambuzi wa Siasa Amboka Andere kutoka nchini Kenya.

Mvutano umekuwa mkubwa tangu kutangazwa kwa mara ya kwanza kwa kifo cha Osama Bin Laden huku wengine wakihoji namna ambavyo zoezi hilo lilivyoendeshwa na wengine wakiwa na shauku ya kushuhudia picha za mwili wa Kiongozi huyo wa zamani wa Al Qaeda.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.