Pata taarifa kuu

Ukraine yazindua ubalozi wake nchini Côte d'Ivoire

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine amezindua ubalozi wa Ukraine nchini Côte d'Ivoire siku ya Alhamisi, baada ya DRC siku ya Jumatano, katika hali ambayo Ukraine inajaribu kukabiliana na ushawishi wa Urusi barani Afrika.

Uzinduzi huu ni "matokeo ya utekelezaji mzuri wa maagizo ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ya kupanua uwepo wa kidiplomasia wa Ukraine barani Afrika", ameongeza.naibu waziri wa Ukraine katika hotuba yake ya uzinduzi huo iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.
Uzinduzi huu ni "matokeo ya utekelezaji mzuri wa maagizo ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ya kupanua uwepo wa kidiplomasia wa Ukraine barani Afrika", ameongeza.naibu waziri wa Ukraine katika hotuba yake ya uzinduzi huo iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP. AP
Matangazo ya kibiashara

Maksym Soubkh, mwakilishi maalum wa Ukraine kwa Mashariki ya Kati na Afrika, amezindua uwakilishi huu wa kidiplomasia katika wilaya ya Cocody, katika mji mkuu wa kiuchumi wa Côte d'Ivoire, Abidjan, shirika la habari la AFP limebaini.

"Ukurasa mpya mzuri unaandikwa katika historia mpya ya uhusiano wa Ukraine na Afrika na Ukraine na Côte d'Ivoire," amekaribisha naibu waziri wa Ukraine katika hotuba yake ya uzinduzi huo iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP. Uzinduzi huu ni "matokeo ya utekelezaji mzuri wa maagizo ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ya kupanua uwepo wa kidiplomasia wa Ukraine barani Afrika", ameongeza.

"Tunaichukulia Côte d'Ivoire kuwa mmoja wa washirika wa kibiashara wa Ukraine wanaoahidi katika Kusini mwa Jangwa la Sahara" na "mmoja wa viongozi katika kanda ya Afrika Magharibi," ameainisha. "Kufunguliwa kwa ubalozi nchini Côte d'Ivoire kunaelezewa na nia yetu ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na washirika wetu, Côte d'Ivoire", hasa katika nyanja ya biashara, kilimo, viwanda, nishati na elimu, amesema.

Katika kujaribu kukabiliana na ushawishi wa Urusi na "kufufua" uhusiano wake na Afrika, Ukraine inapanga kufungua balozi nyingine kadhaa barani humo.

Ubalozi wa Ukraine nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulizinduliwa siku ya Jumatano huko Kinshasa na Bw. Soubkh, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kongo ilithibitisha kwa hirika la habari la AFP. Tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo mwezi wa Februari 2022, mkuu wa diplomasia ya Ukraine Dmytro Kouleba amefanya ziara kadhaa barani Afrika kujaribu kupata msaada dhidi ya Moscow.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Côte d'Ivoire anayehusika na ushirikiano wa Afrika na wa Côte d'Ivoire nje ya nchi, Wautabouna Ouattara, amebaini kwamba uzinduzi huu huko Abidjan "unaonyesha ubora wa uhusiano na ushirikiano unaounganisha nchi zetu mbili tangu kuanzishwa kwa uhusiano wetu wa kidiplomasia mnamo 1992", kulingana na hotuba yake siku ya Alhamisi.

"Ninasalia kuamini kwamba hatua hii mpya katika uhusiano wetu wa kidiplomasia itaongeza ushirikiano wetu kwa kuzingatia uwezo mkubwa na mali nyingi zinazopatikana kwa nchi zetu mbili," ameongeza. Bw. Ouattara amesisitiza tena "uaminifu wa Côte d'Ivoire kwa kanuni za kuheshimu uhuru na uadilifu wa eneo la Ukraine", na anatumai "mwisho wa haraka" wa vita vya Ukraine na "kurejea kwa amani katika eneo hili.

Bw. Soubkh pia alisema "anashukuru sana uungaji mkono wa Côte d'Ivoire kwa mamlaka ya Ukraine na uadilifu wa eneo, hasa kwa kupiga kura kuunga mkono maazimio muhimu ya Umoja wa Mataifa kuhusu uvamizi mkubwa wa Urusi". "Vita hivi vinaweza kuonekana kuwa vya mbali sana kwako, Lakini kupanda kwa bei ya vyakula tayari kumeathiri maisha ya mamilioni ya familia za Kiafrika" hasa, amebainisha.

Naibu waziri wa Ukraine anatarajiwa kusafiri wiki chache zijazo hadi Ghana, Msumbiji, Botswana na Rwanda kuzindua rasmi balozi, kwa mujibu wa mwakilishi wa ubalozi wa Ukraine mjini Abidjan aliyehojiwa na shirika la habari la AFP.

Nchini Rwanda, ubalozi wa Ukraine umefunguliwa tangu Desemba mwaka jana lakini bado haujazinduliwa rasmi na zoezi hili linapaswa kuwa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.