Pata taarifa kuu
USAFIRI -USALAMA

Senegal: Usafiri muhimu wa baharini kati ya Dakar na Casamance waanza tena

Takriban wasafiri 200 wamesafiri kwa furaha kwa feri kati ya Dakar na Casamance (kusini) usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, baada ya miezi kadhaa ya mamlaka kusitisha usafiri huo, uamuzi uliowaumiza raia kufuatia machafuko katika eneo hilo lisilo na bandari.

Feri hiyo haikusafiri ikiwa na abiria wake 484 kwa sababu notisi ya kuanza tena ilikuwa fupi, anasema Oumar Samb. Lakini idadi fulani ya watu walifurahia kusafiri kwa feri hiyo kurudi Casamance, kusheherekea sikukuu kuu ya Korité, jina la ndani lililopewa sikukuu ya Eid al-Fitr kuashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.
Feri hiyo haikusafiri ikiwa na abiria wake 484 kwa sababu notisi ya kuanza tena ilikuwa fupi, anasema Oumar Samb. Lakini idadi fulani ya watu walifurahia kusafiri kwa feri hiyo kurudi Casamance, kusheherekea sikukuu kuu ya Korité, jina la ndani lililopewa sikukuu ya Eid al-Fitr kuashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani. © Raphaëlle Constant/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Tuna furaha sana tena sana kwa sababu tuliteseka sana katika kipindi cha miezi 9," amesema Astou Sané, nesi, ambaye ni miongoni mwa wasafiri. Baada ya kusitishwa kwa usafiri wa feri, "tulisafiri kwa barabara, na mchoko wa kazi. Unapofika, nyumbani au kazini unajihisimgonjwa wa mafua, mchoka."

Feri ya Aline Sitoé Diatta ilisafiri na abiria 233 na mizigo yao kabla ya kuondoka kwenye kwenye kituo chake baada ya giza kuingia, ikipiga honi yake ya ukungu katika bandari ya Dakar, kulingana na meneja wa kituo cha feri, Oumar Samb, na waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP waliokuwepo wa kati feri hiyo ilipong'oa nanga.

Feri hiyo haikusafiri ikiwa na abiria wake 484 kwa sababu notisi ya kuanza tena ilikuwa fupi, anasema Oumar Samb. Lakini idadi fulani ya watu walifurahia kusafiri kwa feri hiyo kurudi Casamance, kusheherekea sikukuu kuu ya Korité, jina la ndani lililopewa sikukuu ya Eid al-Fitr kuashiria mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani. Feri hiyo imepangwa Kuwasili huko Ziguinchor, mji mkuu wa Casamance, Jumatano kabla ya saa sita mchana saa za ndani.

Tikiti ni kuanzia faranga za CFA 5,000 (sawa na euro 7.6), "ni pesa kidogo ikilinganihwa na usafiri wa mabasi ", anasema Alain Théophile Sané, mtafiti wa biolojia ya matibabu. "Tunaweza kulala wakati wa safari, tunafika tumepumzika, safi kabisa. kwa barabara, njia ni ngumu sana, tunafika tumechoka."

Mnamo mwezi Juni 2023, mamlaka ilisitisha safari zilizosimamiwa na boti tatu za kampuni ya Cosama ambayo ilisafirisha mamia ya wasafiri kila wiki kati ya mji mkuu na Casamance, kilomita mia chache kuelekea kusini, kando ya pwani ya Atlantiki katika pande zote mbili. Mamlaka haijatoa maelezo ya kweli. Hatua hiyo ilichukuliwa katika mazingira ya machafuko mabaya ambayo Ziguinchor ilikumbwa nayo, kama vile Dakar na miji mingine, baada ya kuhukumiwa kwa mpinzani wa kisiasa Ousmane Sonko katika kesi ya maadili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.