Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Shule zafungwa mjini Cape Town

Shule zimefungwa katika maeneo ya jimbo la Western Cape nchini Afrika Kusini, ikiwemo mji wa Cape Town, kutokana na dhoruba kali iliyosababisha uharibifu mkubwa katika jimbo hilo.

Mvua kubwa ilionyesha eneo la Durban nchini Afrika Kusini mnamo Aprili 12, 2022.
Mvua kubwa ilionyesha eneo la Durban nchini Afrika Kusini mnamo Aprili 12, 2022. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Kufungwa kwa shule kunaathiri masomo katika maeneo ya Cape Winelands na Overberg, pamoja na eneo la bonde la Helderberg.

Waziri wa Elimu wa Cape Magharibi David Maynier alisema hatua ya kuamua kuzingunga shule kutokana na janga hilo halikuwa rahisi kwani waliona ni bora kuchukuwa taadhari ya mapema kuliko kujutia baadaye.

Mamlaka imewataka wakaazi kuhepuka kuendesha magari na vile vile kuepuka safari zisizo za lazima.

Upepo huo mkubwa pia uliondoa paa, kung'oa miti na kuchochea moto wa nyika, ukaharibu shamba la mvinyo huko Stellenbosch na zaidi ya mali katika eneo la Glencairn.

Upepo huo wa uharibifu unatabiriwa kuendelea Jumatatu. Huduma ya hali ya hewa pia imetoa tahadhari kwa mvua kubwa zinazoweza kusababisha mafuriko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.