Pata taarifa kuu

Senegal: Waziri Mkuu Ousmane Sonko ameunda serikali mpya

Nairobi – Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko, ameunda serikali mpya kwa kuwateua Mawaziri 25 na manaibu Mawaziri watano, siku chache baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo.

Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko
Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa Mawaziri hao, umeidhinishwa na rais Bassirou Diomaye Faye, aliyeapishwa wiki hii, na watakuwa na kazi kubwa ya kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wa Senegal.

Miongoni mwa Mawaziri walioteuliwa ni pamoja na Cheikh Diba, ambaye anakuwa Waziri wa fedha, akiwa na kibarua cha kusimamia ahadi ya rais Faye ya kufanya mageuzi makubwa, hasa nchi hiyo kuachana na matumizi ya CFA franc inayotumiwa na nchi za Afrika Magharibi, zinazozungumza Kifaransa.

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa, rais Faye aliahidi kupitia upya mikataba ya gesi na mafuta, na kazi hiyo amepewa Waziri Birame Souleye Diop, aliyekuwa naibu kiongozi wa cham cha PASTEF, kilichofutwa wakati wa uongozi wa rais wa zamani Macky Sall.

Waziri Mkuu Sonko, amesema baraza hilo la Mawaziri lina sura mpya, wateule ambao watafanya kazi tofauti za serikali iliyopita kwa lengo la kutekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.