Pata taarifa kuu

Sudan: Rais Kiir awaonya wabunge kutong'ang'ania madarakani

Nairobi – Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amewaonya wabunge "kutong'ang'ania madarakani" wiki chache kupita baada ya makamu wake wa kwanza wa rais Riek Machar, kupendekeza kuahirishwa kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu.

Rais wa Sudan Kusini- Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini- Salva Kiir AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Rais Kiir amesema kuongezwa kwa muda wa mpito kutawanyima wananchi fursa ya kuchagua viongozi wao na na sasa amelitaka bunge kupitisha sheria zinazohitajika ili kuandaa njia kuelekea uchaguzi.

Sudan Kusini ilipaswa kufanya uchaguzi kabla ya Februari 2023 lakini ratiba hiyo ilisogezwa mbele hadi mwezi Desemba mwaka huu, ambapo Spika wa Bunge Jemma Nunu Kumba, alisema wabunge wataongeza juhudi kuhakikisha mahitaji yote ya uchaguzi yanatimizwa.

Makamu wa Rais Riek Machar, ambaye vikosi vyake vilipigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika katika mkataba wa amani wa 2018, alipendekeza mwezi uliopita kuongezwa kwa muda wa serikali ya mpito ili kuruhusu maandalizi ya kutosha kwa ajili ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.