Pata taarifa kuu

Makombora yarushwa dhidi ya nyumba ya mpwa wa Waziri Mkuu wa Libya

Roketi mbili zililenga nyumba na ofisi ya mpwa na mshauri wa Waziri Mkuu wa Libya, iliyoko katika eneo la makazi ya mji mkuu wa Libya Tripoli, siku ya Jumapili jioni, na kusababisha uharibifu lakini hakuna majeruhi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Vikosi vya usalama vya Libya wakati wa gwaride la kuadhimisha miaka kumi na tatu tangu kumalizika kwa utawala wa Gaddafi.
Vikosi vya usalama vya Libya wakati wa gwaride la kuadhimisha miaka kumi na tatu tangu kumalizika kwa utawala wa Gaddafi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa televisheni ya al-Wasat, ikinukuu chanzo cha usalama siku ya Jumatatu bila kutaja jina, ofisi na moja ya makazi ya Ibrahim Dbeibah, mpwa wa mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa, zilipigwa na roketi mbili za aina ya RPG. Ibrahim Dbeibah, mshauri wa kisiasa wa Abdelhamid Dbeibah, hakuwepo eneo la tukio wakati wa shambulio hilo, kulingana na chanzo hicho. Hakuna madai yaliyotolewa mara moja na mamlaka huko Tripoli haikutoa maoni yake kufuatia shambulio hilo.

Tangu kuangushwa kwa kiongozi Muammar Gaddafi, aliyeuawa wakati wa uasi mwaka 2011, Libya, iliyoathiriwa na ghasia na migawanyiko ya kindugu, imekuwa ikitawaliwa na serikali mbili hasimu. Moja katika mji wa Tripoli (Magharibi) inaongozwa na Abdelhamid Dbeibah na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine katika Mashariki, imejumuishwa na Bunge na inahusishwa na kambi ya Marshal Haftar, ambayo ngome yake iko Benghazi.

Nyumba na ofisi ya Ibrahim Dbeibah ziko katika eneo lenye usalama zaidi la wilaya ya makazi na biashara ya Hay al-Andalous magharibi mwa Tripoli, pia karibu na jumba la kifahari ambalo Waziri Mkuu Dbeibah hutumia kama ofisi. .

"Milipuko miwili mikubwa ikifuatiwa na milio ya risasi na ving'ora vya polisi" ilisikika Jumapili jioni baada ya kmalizika kwa mfungo wa Ramadhani, kulingana na mkazi wa kitongoji aliyepigiwa simu na shirika la habari la AFP. "Brigade 166" inayohusika na usalama katika sekta hii "ilifunga mara moja barabarani na kuwaita wazima moto," kiliongeza chanzo hiki ambacho kilipendelea kutotajwa jina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.