Pata taarifa kuu

Mfahamu rais mteule wa Senegal Bassirou Diomaye Faye mwenye umri wa miaka 44

Nairobi – Bassirou Diomaye Faye rais mtarajiwa wa Senegal, ambaye amedimisha miaka 44 hapo jana, ni kiongozi ambaye mwaka mmoja uliopita raia wengi wa Senegal hawakuwa wanamtambua.

Kitaluma Faye amesomea maswala ya ukaguzi wa kodi.
Kitaluma Faye amesomea maswala ya ukaguzi wa kodi. REUTERS - Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Faye amefanikiwa kuingia madarakani kutokana na ungaji mkono wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye mamlaka ilimzuia kuwania urais licha ya kwamba aliwavutia sana vijana.

Faye alikuwa naibu wa Sonko katika chama cha Pastef, kabla ya mamlaka kukifuta chama hicho.

Kitaluma Faye amesomea maswala ya ukaguzi wa kodi na alisomea masomo hayo kwenye shule moja na Sonko na pia ametokea katika familia ambao wazazi wake walikuwa wakulima.

Faye hata hivyo hajawahi chaguliwa katika wadhifa wowote wa kisiasa na hii ni mara yake ya kwanza kuchaguliwa
Faye hata hivyo hajawahi chaguliwa katika wadhifa wowote wa kisiasa na hii ni mara yake ya kwanza kuchaguliwa REUTERS - Luc Gnago

Aidha wawili hao walikutana katika mamlaka ya kukagua kodi nchini Senegal na ndipo wakaanzisha chama cha Pastef mwaka 2014.

Marafiki wa karibu wa Faye, wanamsimulia kama tu mwenye msimamo na asiyeshawishika kwa upesi, hilo lilimfanya kuwa ngome katika chama cha Ousmane Sonko.

Faye hata hivyo hajawahi chaguliwa katika wadhifa wowote wa kisiasa na hii ni mara yake ya kwanza kuchaguliwa, na ameahidi kuongoza Senegal kwa kuzingatia sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.