Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Je, uchaguzi wa mwezi Mei Afrika Kusini hautakuwa na dosari?

Je, uchaguzi mkuu wa mwezi Mei nchini Afrika Kusini hautakuwa na dosari? Tume ya uchaguzi na chama tawala cha ANC wanaahidi kuandaa, tofauti na baadhi ya majirani zake, kura inayostahiki demokrasia imara, na kukanusha minong'ono ya "uongo" kutoka kwa upinzani.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Jumamosi hii Februari 24, 2024 katika Uwanja wa Michezo wa Moses Mabhida mjini Durban.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Jumamosi hii Februari 24, 2024 katika Uwanja wa Michezo wa Moses Mabhida mjini Durban. AFP - RAJESH JANTILAL
Matangazo ya kibiashara

Wakati chama cha African National Congress (ANC), chama cha Nelson Mandela, kikiwa katika hatari ya kupoteza kura zake nyingi kwa mara ya kwanza katika historia yake huku kukiwa na minong'ono kwa baadhi ya raia, wiki hii kilitetea uadilifu wa mchakato wa uchaguzi.

Afrika Kusini sio taifa la kizembe, chama kilichoko madarakani kwa miaka thelathini kimesema katika taarifa, wakati chama cha kwanza cha upinzani, Democratic Alliance (DA), kiliomba kuwepo kwa waangalizi wa Marekani katika vituo vya kupigia kura. Takriban wapiga kura milioni 27.8 waliojiandikisha wanaitwa kupiga kura mnamo Mei 29 ili kuwachagua wabunge wapya watakaomteua rais ajaye.

Rais Cyril Ramaphosa alishutumu tabia "mbovu" ya upinzani. Na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Naledi Pandor, amesema kuwa kuomba waangalizi kutoka "nchi ambazo hazina waangalizi (katika chaguzi zao) na ambako ushiriki ni mdogo, ni jambo la kushangaza". Mbinu hii "inafedhehesha" nchi, ameongeza.

Naledi Modise, wa Chuo Kikuu cha Kaskazini-Magharibi, anasema upinzani unaonyesha udhaifu wake katika mzozo huu. Tume ya Uchaguzi (IEC) kwa muda mrefu imeonyesha kuwa ni "chombo kilicho wazi na huru", ambacho "hakiwezi kutiliwa shaka kwa sababu DA inahisi kutishiwa kwa kutotekeleza jukumu hilo na kutofikia malengo yake ya uchaguzi.

Kura za hivi punde zinaipa DA, ikishirikiana na takriban vyama kumi vidogo, makadirio ya hadi karibu 35% ya kura. "Mfumo wetu wa uchaguzi umethibitika kuwa thabiti, wenye uwezo na unaofanya kazi vilivyo," anasema mwanasayansi huyo wa siasa.

Taasisi zenye nguvu

Mkuu wa maswala ya kigeni wa DA, Emma Louise Powell, anahoji kuwa chama chake "kinaiamini IEC katika ngazi ya kitaifa, lakini hitilafu na makosa ya kuhesabu wakati mwingine hutokea ndani ya nchi".

"Ni moja ya tume za uchaguzi zinazoaminika zaidi duniani, na hata zaidi barani Afrika," anabainisha Ongama Mtimka, profesa katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, akibaini kwamba minong'ono ya upinzani inapaswa kuegemea kwenye shqhidi zinazoonekana. Afrika Kusini inadumisha sifa yake ya kuvutia katika bara kama demokrasia ya kupigiwa mfano, na kuandaa chaguzi sita za kitaifa ambazo hazijapingwa.

Tume yake ya uchaguzi, iliyoundwa wakati wa kipindi cha mpito kutoka kwa ubaguzi wa rangi hadi uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1994, inaheshimiwa sana katika nchi ambayo kwa miongo kadhaa ilizuia haki za kupiga kura kwa wazungu wake wachache. "Uaminifu wa tume unatokana na muundo wake na mfumo wake wa kisheria", misingi yake ni thabiti, alisema mwenyekiti wake Sy Mamabolo wiki hii wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

"Afrika Kusini ni nchi huru (...) na tume yake ya uchaguzi ina sifa nzuri ya muda mrefu ya kuandaa uchaguzi huru na wa haki," David Feldmann, msemaji, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.