Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 20 wamefariki katika ajali ya boti ya wahamiaji nchini Senegal

Zaidi ya miili 20 iliopolewa baharini kaskazini mwa Senegal siku ya Jumatano baada ya kuzama kwa boti ya wahamiaji iliyokuwa ikielekea Ulayakulingana na shuhuda, gavana wa eneo la Saint-Louis ameliambia shirika la habari la AFP.

Picha hii iliyotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Uhispania (Cruz Roja) mnamo Julai 13, 2023 inaonyesha mashua ikiwasili katika ufuo wa Las Galletas katika manispaa ya Arona, kwenye kisiwa cha Canary cha Tenerife.
Picha hii iliyotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Uhispania (Cruz Roja) mnamo Julai 13, 2023 inaonyesha mashua ikiwasili katika ufuo wa Las Galletas katika manispaa ya Arona, kwenye kisiwa cha Canary cha Tenerife. © SPANISH RED CROSS / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Zaidi ya miili 20" ilipatikana, amesema Alioune Badara Samb, aliyehojiwa kwa simu. Takriban watu ishirini waliokolewa, ameongeza.

Hakuzungumzia idadi ya abiria waliokuwa kwenye boti hapo awali. Lakini shuhuda kutoka kwa walionusurika zilizokusanywa na mwandishi wa shirika la habari la AFP zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu walikuwa ndani ya boti na kwa hivyo hawakupatikana.

Mamady Dianfo, mwenye asili ya Casamance (kusini ), amesema zaidi ya abiria 300 ambao walikuwa  nadani ya boti hiyo wakati ilipoondoka kwenye pwani ya Senegal wiki moja iliyopita. Mtu mwingine aliyenusurika, Alpha Baldé, amesema abiria walikuwa zaidi ya 200.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.