Pata taarifa kuu

WFP inasema maelfu ya raia wa Sudan hawana chakula

Nairobi – Shirika la umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, linasema miezi kumi tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, maelfu ya raia wa nchi hiyo hawana chakula.

Usambazaji wa chakula katika eneo la Omduman, Sudan, Tarehe 3 Septemba 2023.
Usambazaji wa chakula katika eneo la Omduman, Sudan, Tarehe 3 Septemba 2023. REUTERS - EL TAYEB SIDDIG
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa WFP, wakati huu, chini ya asilimia tano ya raia wa Sudan wanaweza kumudu mlo mmoja pekee, alisema Eddie Rowe, mkuu wa shirika hilo nchini Sudan, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Brussels.

WFP inasema inakabiliwa na ukata huku ikilazimika kusitisha baadhi ya operesheni zake za ugawaji wa chakula kutokana na usalama mdogo kwenye baadhi ya maeneo, ambapo umesababisha raia kushindwa kufanya kilimo cha kujikimu.

Kwa miezi kadhaa sasa Mashirika ya misaada yameonya kuhusu kukwama kwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na ufadhili mdogo wa fedha, hali inayotishia kushuhidiwa kwa baa la njaa kwenye taifa hilo.

Tangu Aprili mwaka jana, Sudan imekuwa ikishihudia mapigano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF, mapigano yaliyosababisha vifo na maelfu kukimbia nchi yao katika kile UN inasema ni moja ya janga baya zaidi la kibinadamu duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.