Pata taarifa kuu

Ufaransa kuwa mwenyeji wa kongamano kuhusu nchi ya Sudan

Nairobi – Ufaransa inasema itakuwa mwenyeji wa kongamano jijini Paris mwezi Aprili mwaka huu kuchangisha fedha za kuisaidia nchi ya Sudan inayokabiliwa na vita.

Raia wa Sudan wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji, dawa na vifa vingine muhimu kutokana na mapigano yanayoendelea.
Raia wa Sudan wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji, dawa na vifa vingine muhimu kutokana na mapigano yanayoendelea. REUTERS - EL TAYEB SIDDIG
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, hali ya kibinadamu kwenye taifa hilo la Afrika haifai kusahulika.

Maelfu ya watu wameuwa nchini Sudan tangu kuzuka kwa mapigano mwaka uliopita mwezi Aprili kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa RSF.

Umoja wa mataifa unaeleza kuwa zaidi ya watu milioni sita wamepoteza makazi yao na kwamba zaidi nusu ya raia wa Sudan wanahitaji msaada.

Licha ya wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan kuendelea kutolewa, pande hasimu zimeonekana kupuuza wito huo, makabiliano yakiendelea kuripotiwa katika maeneo tofauti.

Mazungumzo yamekuwa yakiendelea pia kuzipatanisha pande mbili za kijeshi zinazohasimiana, vikao vya awali vikiripotiwa kukamilika bila ya kuwepo kwa muafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.