Pata taarifa kuu

Kenya: Kiongozi wa dini anakabiliwa na mashtaka 191

Nairobi – Mahakama nchini Kenya imemkuta na makosa 191 ikiwemo mauaji kiongozi wa kidini anayekabiliwa na utata na washirika wake kwa kuhusishwa na vifo vya karibia watu 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya taifa hilo. 

Mackenzie na washirika wake 29 wamekana mashtaka 191 ya mauaji dhidi yao kwa mujibu wa stakabaadhi za mahakama
Mackenzie na washirika wake 29 wamekana mashtaka 191 ya mauaji dhidi yao kwa mujibu wa stakabaadhi za mahakama AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Paul Nthenge Mackenzie, ambaye tayari anakabiliwa na mashtaka mengine ikiwemo ugaidi, kuwatesa watoto, anatuhumiwa kwa kuwashawishi mamia ya wafuasi wake kufunga hadi kufa iliwamuone Yesu.

Mackenzie na washirika wake 29 wamekana mashtaka 191 ya mauaji dhidi yao kwa mujibu wa stakabaadhi za mahakama.

Mshukiwa wa 31 ameagizwa kurejea katika mahakama ya Malindi pwani ya taifa hilo la Afrika Mashariki mwezi ujao baada ya kubainika kuwa hawezi kujibu mashtaka dhidi yake kutokana na changamoto za kiakili.

Paul Nthenge Mackenzie amekana mashtaka dhidi yake
Paul Nthenge Mackenzie amekana mashtaka dhidi yake AFP - -

Kiongozi huyo wa dini alikana mashataka yote dhidi yake.

Mackenzie alikamatwa mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya miili ya watu kupatikana ikiwa imezikwa katika msitu wa Shakahola.

Uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa sehemu kubwa ya waathiriwa 429 walifariki kutokana na njaa.

Mchungaji huyo anatuhumiwa kwa kuwaongoza wafuasi wake kufunga hadi kufa
Mchungaji huyo anatuhumiwa kwa kuwaongoza wafuasi wake kufunga hadi kufa AFP - YASUYOSHI CHIBA

Waathiriwa wengine wakiwemo watoto walithibitishwa kuuawa kwa kupigwa au kunyongwa baadhi wakifa kwa kukosa hewa.

Ikiwa na idadi kubwa ya wakristo, nchi ya Kenya imekabiliwa na changamoto ya kudhibiti makanisa na dini zinazowapotosha watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.