Pata taarifa kuu

Watu 37 wameuawa kwenye eneo linalokabiliwa na mzozo kati ya Khartoum na Juba

Nairobi – Karibia raia 37 wameuawa wengine 18 wakiripotiwa kutekwa katika kisa cha mashambulio mapya kwenye eneo linalokabiliwa na mzozo kati ya Sudan Kusini na Sudan.

Wiki iliopita, makundi mawili ya vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha kutoka katika jimbo la Warrap, walitekeleza shambulio katika jimbo la Abyei ambapo waliwaua watu 53 wakiwemo walinda amani wawili wa UN
Wiki iliopita, makundi mawili ya vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha kutoka katika jimbo la Warrap, walitekeleza shambulio katika jimbo la Abyei ambapo waliwaua watu 53 wakiwemo walinda amani wawili wa UN via REUTERS - VIDEO OBTAINED BY REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya watu waliouawa katika shambulio la wikendi iliopita ni wanawake na watoto kama ilivyoripotiwa na mamlaka ya mpito kwenye eneo hilo.

Aidha kwa mujibu wa mamlaka, soko na makaazi ya watu yalichomwa moto wakati ngombe elfu moja zikiibiwa.

Makundi mawili ya vijana wanaomiliki silaha kutoka katika jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini yamethumiwa kwa mashmbulio yaliopangwa dhidi ya vijiji vinne katika eneo la Abyei.

Waziri wa masula ya mawasiliano na utamaduni katika jimbo la Abyei, Bulis Koch Aguar, amekashifu mashambulio hayo na kutoa wito kwa serikali ya kitaifa ya Juba kuingalia kati kwenye mzozo huo kati ya jamii ya Ngok Dinka kutoka Abyei na Twic Dinka kutoka Warrap.

Wiki iliopita, makundi mawili ya vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha kutoka katika jimbo la Warrap, walitekeleza shambulio katika jimbo la Abyei ambapo waliwaua watu 53 wakiwemo walinda amani wawili wa UN.

Abyei ni jimbo ambalo limekuwa likikabiliwa na mzozo kati ya nchi ya Sudan na Sudan Kusini, mzozo huo ukiwa haujapata suluhu kati ya nchi hizo jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.