Pata taarifa kuu

Mali: Uongozi wa kijeshi waagiza kufungwa kwa kituo cha France 24

Nairobi – Uongozi wa kijeshi nchini Mali, umeagiza kufungwa kwa kituo cha Televisheni cha Ufaransa, France 2, kwa kipindi cha miezi minne kwa kupeperusha ripoti kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Kanali Mamadi Doumbouya, kingozi wa kijeshi nchini Mali
Kanali Mamadi Doumbouya, kingozi wa kijeshi nchini Mali AP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni hatua ya hivi punde kwa Mali, kuendelea kukata ushirikiano wake na mkoloni wake wa zamani Ufaransa, baada ya jeshi kuchukua madaraka mwaka 2021.

Tume ya mawasiliano nchini humo kwenye tangazo lake imesema, ripoti iliyopeperushwa kwenye kituo hicho cha Ufaransa, ililenga kusifu ugaidi.

Pamoja na hilo, ripoti hiyo pia imekosolewa na uongozi wa kijeshi kwa kuwapotosha wananchi kuhusu hali ya usalama nchini Mali na kuwakatisha tamaa, wanajeshi.

Aidha, uongozi huo wa kijeshi, umekishtumu kikosi hicho kwa kuhalalisha uwepo wa kikosi cha Ufaransa cha Barkhane kilichokuwa kinapambana na makundi ya kijihadi, kabla ya kuondoka kwake mwaka 2022.

Kuondoka vikosi vya Barkhane baada ya jeshi nchini Mali kuchukua madaraka mwaka 2020 na 2021, kumeendelea kudhoofisha uhusiano wake na Ufaransa.

Mwaka 2022, uongozi wa jeshi pia ulivingua vituo vingine vya Ufaransa, Televisheni ya France 24 na Idhaa ya  Radio France Internationale.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.