Pata taarifa kuu

Karibia raia milioni nane wametoroka mapigano nchini Sudan: UN

Nairobi – Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa watu karibia milioni nane wametoroka mapigano yanayoendelea nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF.

Mataifa ya Sudan Kusini na Chad ni miongoni mwa nchi zinazowapokea wakimbizi kutoka Sudan
Mataifa ya Sudan Kusini na Chad ni miongoni mwa nchi zinazowapokea wakimbizi kutoka Sudan © Zohra Bensemra / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume inayoshugulikia masuala ya wakimbizi katika Umoja wa Mataifa Filippo Grandi, ambaye anazuru nchi ya Ethiopia, ametoa wito wa misaada zaidi ilikuwasaidia waathiriwa.

Mapigano kati ya kiongozi  wa wanajeshi watiifu kwa mkuu wa jeshi la serikali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani  Mohamed Hamdan Daglo, anayeoongoza kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), yalianza katikati ya mwezi Aprili mwaka jana.

Licha ya juhudi za kidiplomasia kumaliza mapigano hayo kutoka kwa jamii ya kimataifa, muafaka haujapatikana.

Karibia watu milioni nane wameripotiwa kutoroka nchini humo na kuhamia katika mataifa jirani wengine wakiwa wakimbizi wa ndani ya nchi.

Kwa mujibu wa UN, kufikia tarehe 21 ya mwezi Januari mwaka huu, idadi ya watu waliopoteza makazi yao ilikuwa imefikia milioni 7.6 million, nusu ya idadi hiyo wakiwa ni watoto.

Zaidi ya watu laki moja wamehamia nchini Ethiopia mojawapo ya mataifa jirani sita yanayotoa hifadhi kwa wakimbizi kutoka nchini Sudan kwa mujibu wa takwimu za UN.

Aidha idadi ya raia wa Sudan ambao walikimbilia nchini Chad tangu kuanza kwa mapigano hayo ilifikia watu laki tano wiki iliopita. Watu wengine 1500 wakiripotiwa kuingia nchini Sudan Kusini kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.