Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu 50 wameuwa kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini

Nairobi – Watu zaidi ya 50 wakiwemo watoto na wanawake, wameuuawa katika mpaka wa Sudan na Sudan Kusini jimboni Abyei, baada ya kutokea kwa mashambulio yanayoelezwa kuwa mabaya zaidi tangu mwaka 2021.

Hali hii imesababisha mamia ya watu kukimbilia kwenye kambi ya vikosi vya kulinda amani kwa hofu ya kushambimiwa
Hali hii imesababisha mamia ya watu kukimbilia kwenye kambi ya vikosi vya kulinda amani kwa hofu ya kushambimiwa Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha kutoka jimbo la Warrap kutoka Sudan Kusini, waliwavamia watu kwenye jimbo la Abyei, kwa mujibu wa Waziri wa Habari katika jimbo hilo Bulis Koch.

Mbali na raia wa kawaida waliouawa, katika shambulio hilo la mwishoni mwa wiki iliyopita, maafisa wa polisi pia wamepoteza maisha, huku watu wengine 64 wakiachwa na majeraha.

Mwanajeshi wa kulinda amani raia wa Ghana, kutoka kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa naye pia ameuawa katika shambulio hilo, katika kambi ya kijeshi ya Agok.

Hali hii imesababisha mamia ya watu kukimbilia kwenye kambi ya vikosi vya kulinda amani kwa hofu ya kushambimiwa; huku serikali za majimbo ya Abyei na Warrap, zikiapa kufanya uchunguzi wa pamoja kuhusu tukio hili.

Kumeendelea kusuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara kati ya makundi pinzani kutoka kabila la Dinka kuhusu mpaka wa jimbo la Abyei na Warrap kuhusu ni nani anapaswa kukusanya kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.