Pata taarifa kuu

Sudan Kusini inaendelea kuwapokea wakimbizi kutoka Sudan

Nairobi – Sudan Kusini inasema wakimbizi zaidi ya 1300 wanaingia nchini humo kila siku wakitokea katika nchi jirani ya Sudan, ambayo tangu mwezi Aprili mwaka uliopita, imeendelea kushuhudia mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Wakimbizi kutoka Sudan wametorokea katika mataifa jirani ya Sudan Kusini na Chad
Wakimbizi kutoka Sudan wametorokea katika mataifa jirani ya Sudan Kusini na Chad © Zohra Bensemra / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa wakimbizi hao ni Ahmed Awadh, mwenye umri wa miaka ishirini-na-mitano, mwanafunzi wa udaktari katika chuo kikuu cha Khartoum. Amekimbilia jimboni Upper Nile, moja ya majimbo manne yanayowakaribisha raia wa Sudan. 

“Napenda kuishi hapa Sudan Kusini. Kamwe sijisikii kama mkimbizi. Ninajisikia kuwa nyumbani. Familia yangu ingali Sudan kwa sababu ilikuwa vigumu kwa wao kuruhusiwa kupita katika uwanja wa kimataifa wa Juba. “alisema Ahmed Awadh, mmoja wa wakimbizi.

00:14

Ahmed Awadh, mmoja wa wakimbizi

Faheem Suleyman, yeye amekimbilia katika jimbo la Unity. Anasema hajui ni lini atarudi Sudan. 

Tulikuja hapa kutafuta mahali pazuri pa kuishi, mahali salama. Hatujui ni lini vita vitamalizika Sudan.” alieleza Faheem Suleyman.

00:07

Faheem Suleyman

Albino Akol Atak, Waziri anayehusika missada ya binadamu na majanga,katika serikali ya Sudan Kusini, amewamtembelea wakimbizi hao. Anasema hali zao za kibinadamu ni mbaya. 

 “Nilipokuwa kwenye majimbo hayo, hali ilikuwa tete. Pia nilipata wakimbizi wamekwamia huko. Kuwasili kwa wakimbizi kumeongezeka kutokana na kasi ya mapigano Sudan.” alisemaAlbino Akol Atak.

00:22

Albino Akol Atak

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na maswala ya kibinadamu, OCHA, zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni saba-nukta tatu wameyakimbia makaazi yao tangu kuanza vita hivyo mwaka uliopita. 

Ripoti yake James Shimanyula . 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.