Watu 17 wameripotiwa kuuawa katika shambulio Sudan Kusini
Nairobi – Watu 17 wameripotiwa kuuawa nchini Sudan Kusini kwenye jimbo la Jonglei, baada ya vijana waliokuwa na silaha kutoka Duk kushambulia raia. Aidha vijana hao wanadaiwa kuiba zaidi ya ng’ombe elfu saba.
Imechapishwa:
Mapigano haya yamethibitishwa na Peter Lajor Duk kamishena wa kaunti ya Duk, jimboni Jonglei.
“Mapigano makali yalizuka kwenye kaunti ya Duk, mapigano hayo yalisababisha vifo na watu 17 kujeruhiwa.”alisemaPeter Lajor Duk.
Peter Lajor Duk kuhusu Jonglei
Aidha viongozi wa Jonglei, wamelaani mashambulio hayo, wakitaka idara za usalama kuingilia kati, Elizabeth Nyaban anaeleza.
“Waliotekeleza mashambulio hayo ni vijana.” alieleza Elizabeth Nyaban.
Elizabeth Nyaban
Tukio hili linahusishwa na hatua ya vijana wengi kwenye eneo la Pibor kumiliki bunduki kiholela, kama anavyoeleza Abraham Kelang, waziri wa habari wa jimbo hilo.
“Vijana wengi wana bunduki. Ripoti tunayopata si nzuri. Hata hivyo tunalaani vikali kitendo chao cha uhalifu.” alieleza Abraham Kelang.
Peter Lajor Duk kuhusu Jonglei
Majimbo ya Jonglei na Pibor, yamekuwa na utata wa zaidi ya miaka kumi ambako watu wa kabila la Murle hupigana na watu wa kabila la Nuer. Makabila yote ni ya watu wafugaji. Mara kwa mara mapigano yao yanatokana na wizi wa mifugo