Pata taarifa kuu

DRC: Ripoti ya CENCO-ECC MOE yaashiria asilimia 31 ya vituo havikufunguliwa

NAIROBI – Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa CENCO-ECC umetoa ripoti yake ya mchana kuhusu uchaguzi unavyofanyika nchini DRC, na kulingana na ripoti hiyo asilimia 31.37 ya vituo vya kupigia kura havijafunguliwa leo asubuhi, asilimia 45.1 ilipata hitilafu ya vifaa vya Kielektroniki vya kupigia kura.

Raia wamepanga foleni katika kituo kimoja cha kupigia kura nchini DRC, Disemba 20, 2023
Raia wamepanga foleni katika kituo kimoja cha kupigia kura nchini DRC, Disemba 20, 2023 © Chube Ngorombi
Matangazo ya kibiashara

Kadhalika asilimia 9.8 ya vituo vya kupigia kura vilipigwa marufuku kupata waangalizi, huku asilimia 7.84 vilirekodi vitendo vya vurugu vikiwemo vilivyoharibiwa.

Ripoti hiyo imeendelea kusema mvua ilitatiza shughuli katika asilimia 3.92 ya ofisi.

Waangalizi hawa wa CENCO-ECC MOE, wamesema ripoti hii inatokana na takwimu zilizopokelewa kutoka kwa asilimia 22.1 ya waangalizi wake waliotumwa katika miji na maeneo mengine ya vijijini.

Ujumbe huu wa waangalizi, unaitaka CENI kufafanua msimamo wake kuhusu vituo ambavyo havikufunguliwa na ambavyo vilichelewa kufunguliwa, kwa lengo la kuheshimu ibara ya 52 ya sheria ya uchaguzi.

Pia ujumbe huu unapendekeza serikali, kuhakikisha usalama wa raia, mawakala wa CENI na vifaa vya uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura.

Ujumbe mwingine wa uangalizi wa kitaifa, Muungano wa misheni ya waangalizi wa uchaguzi (Symocel) ilitayarisha ripoti ya awali kufuatia maoni kutoka kwa maeneo mbalimbali kunakofanyika uchaguzi. Hitilafu nyingi zimeripotiwa katika mikoa kadhaa ya nchi: kucheleweshwa kwa ufunguzi wa ofisi huko Kinshasa na Sankuru, ukosefu wa vifaa na utendakazi wa mfumo wa upigaji kura huko Haut-Lomani au hata kuchelewa kuwasili kwa vifaa huko Kasaï-Oriental.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.