Pata taarifa kuu
ELIMU-USALAMA

Niger: Serikali yafungua tena shule Tillabéri

Mamlaka mpya zimeanza kufungua tena shule zilizofungwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama huko Tillabéri, eneo la kusini-magharibi ambalo hukabiliwa na ghasia za makundi yenye silaha mara kwa mara. Zaidi ya shule 800 bado zimefungwa. Mamlaka mpya za Niger zinaangazia umuhimu wa kuwahakikishia watoto haki ya elimu. Changamoto katika suala la usalama na vifaa.

Ramani inayoonyesha mji wa Tillabéri nchini Niger.
Ramani inayoonyesha mji wa Tillabéri nchini Niger. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Kufikia mwanzoni mwa mwezi wa Januari, shule 122 zitakuwa zimefunguliwa tena, kulingana na kurugenzi ya elimu ya eneo la Tillabéri iliyonukuliwa na vyombo vya habari vya ndani. Shule hizo zinakuja kujiongeza kwa shule 37 ambazo tayari zimefunguliwa tena. Katika eneo hili la kusini-magharibi, zaidi ya shule 800 bado wamefungwa. Zingine zimefungwa kwa miaka 3 hadi 4 sasa kutokana na ghasia za makundi yenye silaha.

Mamlaka mpya za Niger zinasema kuwa uamuzi wa kufungua upya haukuchukuliwa kirahisi na kuangazia umuhimu wa haki ya watoto ya kupata elimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.