Pata taarifa kuu

Misri: Abdel Fattah al-Sisi kuiongoza nchi kwa muhula wa tatu

NAIROBI – Tume ya kitaifa ya uchaguzi nchini Misri, Jumatatu, Disemba 18, 2023, imemtangaza Rais Abdel Fattah al-Sisi, kama mshindi wa uchaguzi uliopita kwa asilimia 89.6 ya kura.

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, Jumatano, Disemba 14, 2022 huko Washington.
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, Jumatano, Disemba 14, 2022 huko Washington. AP - Mandel Ngan
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu unampatia Sisi mwenye umri wa miaka 69 muhula wake wa tatu na, kwa mujibu wa katiba ya Misri, muhula wa mwisho madarakani, kuanzia Aprili utakaodumu kwa miaka sita.

Katika uchaguzi wa mwaka 2014 na 2018, Sisi alishinda kwa zaidi ya asilimia 96 ya kura.

Ushindi wake unakuja licha ya msukosuko wa kiuchumi, unaotokana na kushuka kwa thamani ya sarafu na kuongezeka kwa mvutano wa kikanda uliosababishwa na vita vya Israel na Hamas katika eneo jirani la Gaza.

Wagombea wengine

Hazem Omar, wa chama cha Republican People's Party, ameibuka wa pili kwa asilimia 4.5 ya kura.

Wengine ni Farid Zahran wa chama cha Egyptian Social Democratic Party, na Abdel-Sanad Yamama kutoka chama cha Wafd.

Tume ya uchaguzi imesema idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 66.8 ya wapiga kura milioni 67, idadi ambayo iliongezeka kutoka asilimia 41 mwaka 2018 na asilimia 47 mwaka 2014.

Tathmni ya uongozi wa Sisi

Ni katika uongozi wake ambapo alibadilisha miaka ya muhula wa urais kutoka 4 hadi 6 na kubadilisha katiba.

Utawala wake pia umeshuhudia makumi kwa maelfu ya wanasiasa wa upinzani wakikamatwa na kufungwa jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.