Pata taarifa kuu

Senegal: Mahakama yamuidhinisha Ousmane Sonko kuwania urais mwakani

NAIROBI – Kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, sasa atawania urais wa nchi hiyo mwaka ujao, baada ya mahakama kuagiza jina lake kurejeshwa kwenye sajili ya wapiga kura.

L'opposant sénégalais Ousmane Sonko à Dakar en mars 2021.
L'opposant sénégalais Ousmane Sonko à Dakar en mars 2021. AP - Sylvain Cherkaoui
Matangazo ya kibiashara

Jaji katika mahakama ya Dakar, Alhamisi, Disemba 14, ametoa uamuzi unaowiana na ule uliotolewa mwezi Oktoba na mahakama mjini Ziguinchor, ambako Sonko alikuwa meya.

Sonko amabye anaendelea kutumikia kifucho chake gerezani, aliondolewa kwenye daftari la wapiga kura baada ya mwezi Juni kuhukumiwa miaka 2 jela kwa madai ya kuwapotosha vijana kimaadili, huku kukishuhudiwa misururu ya maandamano yenye vurugu nchini humo.

Kiongozi huyo wa upinzani, sasa ana hadi Disemba 26, kuwasilisha stakabadhi zake za kugombea katika uchaguzi wa Februari. 

Mmoja wa mawakili wake, Cire Cledor Ly, amesema serikali inaweza ikakata rufaa uamuzi huo lakini hilo halitazuia uamuzi wa hivi leo kutekelezwa mara moja.

Kanuni za uchaguzi ziko wazi sana. Jaji akitoa uamuzi wake, uamuzi huu lazima ufanyike mara moja, amesema Ly.

Sonko mwenye umri wa miaka 40, katika hukumu ya miaka miwili jela mwezi Juni hakuwepo mahakamani, na alituhumu hukumu hiyo akisema ni njama ya kumzuia ili asiwanie katika uchaguzi ujao.

Mwishoni mwa Julai, Sonko alikamatwa kwa mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na kuchochea uasi, kujihusisha na uhalifu wa kigaidi na kuhatarisha usalama wa serikali na tangu afungwe jela, mara kwa mara amekuwa kwenye mgomo wa kula.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.