Pata taarifa kuu

Washington inapongeza mwaka wa "rekodi" kwa biashara na Afrika

Marekani imekaribisha siku ya Jumatano kuhitimishwa kwa makubaliano ya rekodi ya kibiashara na Afrika mwaka huu, ya jumla ya dola bilioni 14.2, katika muktadha wa mapambano ya ushawishi na China katika bara hilo.

Mbele ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, bango linaloashiria mkutano wa kwanza wa kilele wa Marekani na Afrika, uliofanyika kuanzia Agosti 4.
Mbele ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, bango linaloashiria mkutano wa kwanza wa kilele wa Marekani na Afrika, uliofanyika kuanzia Agosti 4. AFP/Paul J. Richards
Matangazo ya kibiashara

Takriban mikataba mipya 550 ya biashara na uwekezaji imetiwa saini, ikiwakilisha ongezeko la 67% ikilinganishwa na mwaka 2022 kwa idadi na thamani, amesema British Robinson, mratibu wa mpango wa biashara wa "Prosper Africa" ​​uliozinduliwa na Marekani.

"Tulikuwa na mwaka wa 'rekodi' kwa uhusiano wa Marekani na Afrika," amesema Judd Devermont, mkuu wa Ikulu ya White House Kusini mwa Jangwa la Sahara, wakati wa mkutano wa mtandaoni ulioandaliwa mwaka mmoja baada ya mkutano na viongozi wa Afrika ambapo Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi "kuongeza uhusiano tosha" wa Marekani kwa Afrika.

Washington ilijitolea mwezi Desemba kuwekeza dola bilioni 55 kwa miaka mitatu barani Afrika. Mkakati huu unalenga hasa kukabiliana na ongezeko la uwepo wa China, ambayo imejiingiza katika ujenzi wa miundombinu, uwekezaji na mikopo.

Marekani tayari imefanikisha zaidi ya 40% ya ahadi hizi, amesisitiza Bw. Devermont. "Mwishoni mwa mwaka wa pili, tunapanga kuzidi angalau 70% ya malengo yetu," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.