Senegal: Ousmane Sonko kujua hatma yake kuwania urais mwakani
NAIROBI – Mahakama nchini Senegal inatarajiwa kufanya uamuzi hii leo kuhusu hatima ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko aliyeondolewa kwenye orodha ya wagombea Urais kufuatia uchaguzi wa mapema mwaka ujao.
Imechapishwa:
Cheza - 00:48
Hii leo mahakama ya Dakar nchini Senegal itaamua endapo kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko, anapaswa kurudishwa katika daftari la uchaguzi, hatua ambayo itaamua kuhusu hatima yake ya kugombea uchaguzi ujao wa rais.
Kiongozi huyo wa upinzani aliondolewa kwenye daftari la uchaguzi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mwezi Juni baada ya kupatikana na hatia ya kuwapotosha vijana kimaadili.
Mwanasiasa huyo amekuwa katikati ya mvutano na serikali kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili, hali iliyozusha machafuko mara kadhaa nchini Senegal.
Sonko anadai kesi zinazomuandama zimeundwa, kwa lengo la kumzuia kugombea uchaguzi wa rais,madai ambayo serikali imeyakanusha ikisema haina ushawishi katika mfumo wa mahakama.