Pata taarifa kuu

Wanasheria wa Uingereza kuelekea Rwanda kuhusu mpango wa waomba hifadhi

Nairobi – Wanasheria wa Uingereza, huenda wakatumwa nchini Rwanda, kama sehemu ya mkataba mpya unaolenga kutekeleza mpango wa Serikali ya waziri mkuu Rishi Sunak, kuwapeleka wahamiaji kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly anaondoka 10 Downing Street baada ya kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri, London, Jumanne, Novemba 28, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly anaondoka 10 Downing Street baada ya kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri, London, Jumanne, Novemba 28, 2023. AP - Kirsty Wigglesworth
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza James Cleverly, amethibitisha hilo, wakati huu wakiwa katika harakati za mwisho za kukamilisha mkataba na Rwanda na kuufanya mpango huo kuwa halali.

Haya yanajiri huku wanasheria na mashirika ya misaada yakiamini kuwa ndege yenye waomba hifadhi haitapaa kuelekea Rwanda kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Cleverly anatarajiwa kuelekea nchini Rwanda wiki hii kutia saini mkataba huo, huku sheria za ndani pia zikirekebishwa ili bunge la Uingereza lithibitishe kuwa Rwanda ni mahali salama kwa waomba hifadhi wanaofika Uingereza.

Baada ya uamuzi wa mahakama tarehe 15 Novemba, serikali imekuwa ikijaribu kutafuta mbinu nyingine kuwapeleka wahamiaji hao Rwanda, na kumekuwa na ripoti kwamba Rwanda inashinikiza kupewa fedha zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.