Pata taarifa kuu

DRC: Watoto zaidi ya 170 wameondolewa katika makundi yenye silaha

Nairobi – Taasisi ya kitaifa inayojihusisha na mpango wa kuondoa watoto jeshini na kuwarejesha katika maisha ya kawaida katika jamii (PDDRC-S) imesema kuwa zaidi ya watoto 170 wamekwisha ondolewa kutoka makundi yenye silaha yaliyoko  eneo la Kalehe mkoani Kivu Kusini) mashariki mwa DRC.

Makundi yenye silaha kama vile M23 yamekuwa yakituhumiwa kwa kuwasajili watoto kwenye vikosi vyao
Makundi yenye silaha kama vile M23 yamekuwa yakituhumiwa kwa kuwasajili watoto kwenye vikosi vyao AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyochapishwa hapo jana siku ya Jumanne, taasisi hiyo inayojihusisha na mpango wa kuwaondoa wapiganaji wanaodhihirisha utashi wao wa kuachana na shughuli za kijeshi wakitaka kurejeshwa katika jamii unaofahamika kama (PDDRC-S) ni kuwa jumla ya watoto 172 waliondolewa wiki jana kutoka kwa makundi yenye silaha raia Mutomboki Kirikou, Butachibera na Bibilo. Miongoni mwao ni wasichana 45.

Kuondolewa kwa watoto hawa wanaohusishwa na makundi yenye silaha ni matokeo ya jitihada za kuimarisha mpango huu na washirika wa taasisi hii wanaopigania haki za watoto na wababe wa vita.

Baada ya kuondolewa katika makundi yenye silaha maeneo ya Kalehe huko Kivu kusini, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo watoto hawa, wamewekwa katika familia za wenyeji kwa muda mfupi kwa ajili ya matunzo ya kisaikolojia kabla ya kuunganishwa na jamii.

Shughuli hizi zinafadhiliwa na shirika la umoja wa mataifa linalowashughulikia watoto ulimwenguni, UNICEF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.