EAC: Ufadhili wapungua mabadiliko ya hali ya hewa yakiendelea kushuhudiwa
Nairobi – Misaada ya kibinadamu imeonekana kuaanza kupungua katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki wakati huu zinapokabiliwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, karibia watu 130 katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mataifa yalio kwenye pembe ya Afrika ndiyo yameathirika zaidi na mafuriko hayo yanayoshuhudiwa baada ya kukabiliwa na ukame wa muda mrefu zaidi katika kipindi cha miaka 40.
Licha ya kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa misaada ya kibindamu katika nchi hizo tatu za Kenya, Somalia na Ethiopia, misaada hiyo imeripotiwa kupungua kwa Dolla bilioni 4.1 tangu mwazoni mwa mwaka huu peke.
Inahofiwa kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi haswa wakati huu wahisani kama vile Uingereza, Canada na Ujerumani zikipanga kupunguza ufadhili wake mwaka ujao kwa asilimia 50.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la misaada la Oxfam, mataifa tajiri duniani yalilipa chini ya asilimia tano peke ya Dolla bilioni 53.3 kwa mataifa ya Afrika Mashariki kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa sasa mataifa ya Kenya, Somalia na Ethiopia yanahitaji bilioni saba kwa pamoja ilikuwasaidia waathiriwa wa mabadiliko ya hali ya hewa japokuwa ni asilimia 41 peke ya ufadhili ambayo imepatikana.
Nchini Somalia, zaidi ya watu milioni moja wameathirika na mafuriko baada ya mto Juba na Shabelle kuvunja kingo zake na kuharibu makazi yao.
Haya yanajiri wakati huu mafuriko yakiwa yamesababisha vifo vya watu 52 nchini Kenya, familia zaidi elfu 15 zikipoteza makazi yao, hali sawia ikiripotiwa nchini Ethiopia.