Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire Guillaume Soro akutana na Jenerali Tiani mjini Niamey

Waziri mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire Guillaume Soro, ambaye siku ya Jumapili alitangaza kwamba anarejea nchini baada ya kukimbilia uhamishoni  tangu mwaka 2019, amekutana siku ya Jumatatu huko Niger na Jenerali Abdourahamane Tiani, ambaye aliingia madarakani kupitia mapinduzi mnamo mwezi Julai.

Guillaume Soro (picha ya kumbukumbu).
Guillaume Soro (picha ya kumbukumbu). Lionel BONAVENTURE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Nilipata heshima ya kupokelewa leo kwenye hadhara na Rais wa Mpito wa Niger, Mkuu wa Nchi, Jenerali Abdourahamane Tiani, akiandamana na Jenerali Salifou Mody, Waziri wa Ulinzi na Jenerali Mohamed Toumba, Waziri wa Mambo ya Ndani," amesema. Bw. Soro kwenye akaunti yake ya X (zamani ikiitwa Twitter).

"Mazungumzo, ambayo yalichukua saa moja na nusu, yalikuwa ya kipekee katika suala la ubora na kina cha mazungumzo," ameongeza.

Mapema asubuhi, Bw. Soro alitangaza kuwa yuko Niamey tangu siku ya Jumamosi.

Siku ya Jumapili jioni alitangaza kwamba alimeamua kurejea nchini mwake, akibaini kwamba ilikuwa "uchungu kwake kuishi mbali" na "nchi yake ya asili na alikozaliwa Afrika".

Hata hivyo, hakutaja tarehe ya uwezekano wa kurejea nchini Côte d'Ivoire, ambako anakabiliwa na kifungo cha maisha.

Guillaume Soro, kiongozi wa zamani wa waasi ambao walidhibiti nusu ya kaskazini ya Côte d'Ivoire katika miaka ya 2000, na kisha Waziri Mkuu na spika wa Bunge la Kitaifa, alikosana na Alassane Ouattara mnamo mwaka 2019 na ameishi uhamishoni tangu wakati huo.

Alihukumiwa mwaka 2020 akiwa hayupo kifungo cha miaka 20 jela kwa "ubadhirifu wa fedha za umma" nchini Côte d'Ivoire, kisha kifungo cha maisha mwaka mmoja baadaye kwa "kuhatarisha usalama wa taifa".

Wiki chache baada ya mapinduzi ya Julai 26 nchini Niger, Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara alikuwa miongoni mwa viongozi walio na msimamo mkali wa nchi za Afrika Magharibi kuunga mkono uingiliaji kati wa kijeshi kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.