Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

DRC: Roger Lumbala anayeshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu atahukumiwa nchini Ufaransa

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu, majaji wa Ufaransa walizingatia kwamba wana  ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Kongo, Roger Lumbala. Alikuwa kiongozi wa kundi lenye silaha la RCD-N wakati wa Vita vya Pili vya Kongo.

Aliyekuwa mbabe wa kivita wa Kongo Roger Lumbala alikamatwa mjini Paris na kufunguliwa mashtaka mwaka wa 2021.
Aliyekuwa mbabe wa kivita wa Kongo Roger Lumbala alikamatwa mjini Paris na kufunguliwa mashtaka mwaka wa 2021. © AFP/ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Roger Lumbala atahukumiwa kwa kuhusika katika uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa mwaka 2002 na 2003 huko Ituri na Kivu Kaskazini. Shtaka hili linakuja mwishoni mwa karibu miaka mitatu ya uchunguzi, ambapo licha ya hali ya kuzingirwa na vikwazo vilivyohusishwa na Uviko, waathiriwa, wakiungwa mkono na mashirika yasiyo ya kiserikali, waliweza kutoa ushahidi.

Miaka 20 baada ya mshutuko na huzuni, waathiriwa waliondoka kwenye vijiji vyao na kusafiri hadi Ufaransa na kuwaambia wachunguzi kuhusu mauaji, ubakaji na uporaji ulioshuhudiwa wakati wa kampeni mbaya ya "Futa Picha". Operesheni iliyofanywa mwishoni mwa mwaka 2002 na mwanzoni mwa mwaka 2003, katika miezi ya mwisho ya vita vya pili vya Kongo, na kundi lenye silaha la RCD-N na washirika wake (pamoja na MLC) kuchukua udhibiti wa maeneo ya mashariki mwa DRC.

Kwa mujibu wa Daniele Perissi, mkuu wa mpango wa DRC waTrial International DRC, ujasiri huu wa waathiriwa ni wa kushangaza: "Ilihitaji ujasiri kusafiri kilomita elfu kadhaa, kuweza kuelezea uhalifu huu mbele ya jaji na wachunguzi kutoka tamaduni nyingine, katika nchi nyingine. Hii inaonesha kidogo mamlaka ya ulimwengu ni nini: uhalifu wa kutisha, wa kikatili unaweza na unapaswa kutoa nafasi ya uchunguzi na kesi katika nchi yoyote duniani, ikiwa nchi ambayo uhalifu ulifanyika haiwatendei haki waathiriwa. "

Ushuhuda huu uliokusanywa na wachunguzi wa Ufaransa wakati wa awamu ya uchunguzi, ambayo ilianza mapema mwaka 2021, iliongezwa kwenye nyaraka zilizopo: hasa ripoti ya Umoja wa Mataifa (Rapport Mapping) ambayo ilibainisha mamia ya mauaji yaliyofanywa kati ya mwaka 1993 na 2003 nchini DRC.

Wachunguzi wa Ufaransa pia waliweza kutegemea ripoti kutoka kwa Kundi la Haki za Wachache, shirika lisilo la kiserikali ambalo lilifanya kazi hasa na mashirika ya Kongo juu ya uhalifu uliofanywa dhidi ya jamii ya kiasili ya Bambouti.

Wakili wa Cameroon Samuel Ade ni msemaji wa Kundi la Haki za Wachache katika suala hili. “Tulisaidia waathiriwa kusafiri ili watoe ushahidi wa maovu waliyoyapata kwa wachunguzi, ili waliohusika na uchunguzi wawe na ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka Roger Lumbala. Ilikuwa ngumu. Kwa sababu jamii ya Bambouti inaishi katika eneo hatari ambapo makundi mengi yenye silaha yanaendesha uovu wao. Imechangiwa na mazingira ya usalama, ambayo pia ni magumu kwa waathiriwa ambao hawajazoea kusafiri. Pia, kwao, ilikuwa ni kujaribu kusimulia ukatili uliowasibu. Shitaka hili leo ni muhimu. Hii ni ishara muhimu sana. Waathiriwa wanatumai haki na fidia. Hii ina maana fidia na hakikisho kwamba uhalifu huu hautarudiwa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.