Pata taarifa kuu

Sudan: Jeshi na wapiganaji wa RSF wameonesha nia ya kurahisisha utoaji wa misaada ya kibinadamu

Nairobi – Shirika la habari la umma nchini Saudi Arabia, limeripoti kuwa ujumbe wa Serikali ya kijeshi ya Sudan na ule wa wapiganaji wa RSF, wameonesha nia ya kurahisisha utoaji wa misaada ya kibinadamu, ingawa hawajakubali kusitisha mapigano.

À gauche, le chef des forces armées soudanaises, le général al-Burhan et à droite celui des Forces de soutien rapide, le général Hemedti.
À gauche, le chef des forces armées soudanaises, le général al-Burhan et à droite celui des Forces de soutien rapide, le général Hemedti. AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Pande hizo mbili, ambazo zimekuwa zikipigana tangu Aprili, hapo awali zilikubaliana lakini mwishowe zilikiuka makubaliano ya usitishaji mapigano na ahadi za kuwezesha misaada na kulinda raia.

Mpango huo uliotangazwa na wapatanishi haujumuishi usitishaji vita na hivyo hautearajiwi kupunguza mapigano.

Mapigano katika jimbo la Darfur na mji mkuu Khartoum yameshika kasi tangu pande hizo zilipoanza kukutana tena mwezi uliopita kwa mazungumzo, yanayoratibiwa na Saudi Arabia, Marekani na jumuiya ya kikanda IGAD.

Wakati haya yakijiri, wapiganaji wa RSF wamekuwa wakinyooshewa kidole kwa kile kinachoelezwa kuanzisha upya mapigano ya kikabila kwenye jimbo la Darfur, licha ya kundi hilo kukana.

Hata hivyo katika taarifa yao, wapatanishi wameonesha kusikitishwa na pande hizo kushindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.