Pata taarifa kuu

Kongamano kuhusu afya ya umma la mwaka huu CPHIA 2023 linafanyika jijini Lusaka

Nairobi – Mkutano wa kila mwaka wa kimataifa wa afya ya umma barani Afrika (CPHIA) linaandaliwa na kituo cha  Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (Africa CDC) na hutoa nafasi ya kipekee kwa raia wa bara Afriaka pamoja na viongozi kutoka kwenye maeneo tofauti kutafakari mafunzo waliyopata katika afya na sayansi pamoja na kupanga namna ya kuunda mifumo thabiti zaidi ya afya.

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu afya ya umma barani Afrika
Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu afya ya umma barani Afrika © cphia2023
Matangazo ya kibiashara

CPHIA 2023 ni kikao cha tatu kinachojiri baada ya  mkutano uliofanyika kwa njia ya video mnamo mwaka wa 2021  na mwengine uliowakutanisha washika dau katika sekta ya afya jijini Kigali, Rwanda, mnamo 2022.

Mwaka huu, wizara ya afya nchini Zambia ndio itakuwa mwenyeji wa CPHIA 2023 mwezi huu wa Novemba kati ya tarehe 27-30 katika jiji la Lusaka.

CPHIA 2023 itafanyika ana kwa ana mjini Lusaka, Zambia katika barabara ya Kenneth Kaunda katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mulungushi.

Iwapo unataka kujisajili unaweza kutembelea wavuti wa Cphia2023 kwa maelezo zaidi.Kwa kuzingatia maazimio ya mwaka uliopita, CPHIA 2023 inalenga kuonyesha namna  bara la Afrika lilivyokabiliana na kuondoa vizuizi pamoja na kudhibitisha tena Afrika kama kituo chenye uwezo katika sayansi na uvumbuzi.

Kongamano hilo pia linatarajiwa kutoa nafasi kwa vijana wa bara Afrika.

Aidha kikao cha mwaka huu kinalenga kuonyesha jinsi Afrika inauwezo wa kuzindua maarifa mapya na bidhaa za afya pamoja na kuwa kielelezo cha maendeleo.

Mkutano wa mwaka huu unakuja wakati huu mataifa ya Afrika yakiwa mbioni kujiweka sawa katika sekta ya afya ya umma haswa baada ya mlipuko wa uviko 19 ambapo sasa CPHIA inalenga kusaidia kujenga Afrika yenye mifumo bora ya afya, yenye ustawi zaidi katika ukanda wa Afrika na kidunia.

Malengo ya kongamno la mwaka huu CPHIA2023:

Utayari wa kukabiliana na majanga pamoja na mikakati ya ufadhili kwa bara Afrika.

Kuimarisha na kuinua ubunifu wa bara Afrika pamoja na kuendeleza  uzalishaji wa chanjo za ndani ya bara, uchunguzi wa magonjwa na upatikanaji wa tiba.

Kutoa nafasi ya upatikanaji wa afya kwa wote katika bara Afrika, kutilia nguvu usawa katika mifumo ya kiafya kwenye bara.

Kongamano la mwaka huu linafanyika nchini Zambia tarehe 27 hadi tarehe 30 ya mwezi huu
Kongamano la mwaka huu linafanyika nchini Zambia tarehe 27 hadi tarehe 30 ya mwezi huu © CPHIA2023

Upatikanji wa afya ya kutosha kwa wanawake, wasichana na wanawake wachanga barani Afrika.

Kubadilisha sekta ya afya barani Afrika kwa kutumia uvumbuzi wa kidigitali.

Kukabiliana na magonjwa ya kuambukizana barani Afrika pamoja na kushugulikia suala la afya ya akili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.