Pata taarifa kuu

Miaka 10 tangu kuuawa kwa wanahabari wa RFI Kifaransa Ghislaine Dupont na Claude Verlon

Nairobi – Leo ni maadhimisho ya miaka 10 kamili tangu kuuawa kwa wanahabari wa RFI Kifaransa Ghislaine Dupont na Claude Verlon mikononi mwa wanajihadi  wanaoshirikiana na Al Qaeda huko Kidali, Kaskazini mwa Mali.

Kundi la Al Qaeda katika eneo la Maghreb lilikiri kuhusika na mauaji hayo. Waliwateka na baadaye kuwauwa wanahabari hao
Kundi la Al Qaeda katika eneo la Maghreb lilikiri kuhusika na mauaji hayo. Waliwateka na baadaye kuwauwa wanahabari hao RFI
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al Qaeda katika eneo la Maghreb lilikiri kuhusika na mauaji hayo. Waliwateka na baadaye kuwauwa wanahabari hao.

Miaka 10 baadaye, familia za wanahabari hao bado zina maswali mengi, kuhusu kilichojiri. Uchunguzi bado unaendelea nchini Ufaransa, huku wapendwa walioachwa nyuma wakitumai kuwa haki itatendeka.

Marie-Solange Poinsot ni mama yake mzazi, Ghislaine Dupont.

‘Nina kumbukumbu mbaya sana, kwangu mimi tangu miaka kumi iliyopita nimekuwa nikimlia binti yangu, alikuwa ni mwanangu wa mwisho na alikuwa na upendo sana.’’ alisema Marie-Solange Poinsot ni mama yake mzazi, Ghislaine Dupont.

00:21

Marie-Solange Poinsot ni mama yake mzazi, Ghislaine Dupont

Wakati huu uchunguzi ukiendelea, ambapo watalaam wanachunguza mawasiliano ya simu ya watekaji, uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Mali, unaelezwa kuyumbisha uchunguzi huo, wakati huu familia zikiendelea kusubiri kufahamu ukweli.

Apolline Verlon ni binti yake, Claude Verlon.

‘‘Ningependa kumpata mtu atakaye ni hadithia dakika nini kilichotokea ilikukweli ufahamike, ninahisi kwamba kuna mambo hawajatuambia.’’ alisema Apolline Verlon ni binti yake, Claude Verlon.

00:27

Apolline Verlon ni binti yake, Claude Verlon

Baada ya mauaji hayo ya wanahabari hao wa RFI, Umoja wa Mataifa ulitangaza kila tarehe 2 Novemba, kuwa siku ya Kimataifa ya kupambana na kumaliza makosa ya jinai dhidi ya wanahabari duniani, kwa kumbukumbu ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.