Pata taarifa kuu

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umekumba majimbo matatu ya Sudan

Takriban visa 817 vinavyoshukiwa kuwa maradhi ya kipindupindu vimeripotiwa katika majimbo matatu ya Sudan, vikiwemo vifo 35.

Wanawake wa Sudan wanapokea matibabu katika hospitali ya shamba huko Adré, Chad, kwenye mpaka na Sudan.
Wanawake wa Sudan wanapokea matibabu katika hospitali ya shamba huko Adré, Chad, kwenye mpaka na Sudan. © Mohaned Belal / AFP
Matangazo ya kibiashara

Visa hivyo viliripotiwa katika majimbo ya Gedaref, Kordofan Kusini na Khartoum, tovuti ya habari inayomilikiwa kibinafsi ya al-Rakoba iliripoti, ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulisema kuwa miezi kadhaa ya migogoro nchini Sudan imewaacha mamilioni ya watu katika hatari ya ugonjwa wa kipindupindu, surua, malaria na magonjwa mengine bila uwezo wa kutosha wa kujizuia.

WHO pia imeonya kwamba maisha ya zaidi ya wagonjwa 9,000 wa figo yako hatarini kutokana na idadi ndogo ya vituo vya kusafisha damu nchini humo.

Hospitali za Sudan zimeathiriwa pakubwa na mzozo kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi, huku nyingi zikisimamisha shughuli huku kukiwa na mapigano.

Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000 na wengine karibu milioni sita kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.