Pata taarifa kuu

Niger:Msafara mwingine wa wanajeshi wa Ufaransa kuondoka siku chache zijazo

Msafara mwingine wa wanajeshi wa Ufaransa unatarajiwa kuondoka Niger kuelekea Chad, katika siku chache zijazo, hatua inayoashiria kutimia kwa ahadi ya Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake karibu elfu 1 na 400 walioko Niamey.

Wiki iliyopita msururu wa mabasi ulionekana kuwabeba wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa kusini magharibi mwa Niger
Wiki iliyopita msururu wa mabasi ulionekana kuwabeba wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa kusini magharibi mwa Niger AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kanali Mamane Sani Kaiou wa jeshi la Niger, mpango wa kuondoka kwa wanajeshi wengine wa Ufaransa, kutafanya mchakato huo kufikia karibu nusu ya wanajeshi wote waliokuwa nchini humo.

Wiki iliyopita msururu wa mabasi ulionekana kuwabeba wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa kusini magharibi mwa Niger, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya utawala wa kijeshi ambao umeamua kusitisha ushirikiano wa kiusalama na Paris.

Kanali mamane, amesema tayari watu 282 wameshaondoka na kwamba katika siku chache zijazo, wengine zaidi ya 400 wataondoka ambapo watafanya wanajeshi wa Ufaransa wtakaokuwa wamesalia nchini humo kuwa elfu 1 na 450.

Aidha kamanda wa vikosi vya Ufaransa, Jenerali Eric Ozanne, amesema askari walioondoka wiki iliyopita wameshafika mjini Njamena na kwamba watahakikisha wanajeshi wake wote wameondoka nchini humo kufikia Desemba 31 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.