Pata taarifa kuu

Niger: Jeshi linasema limezuia jaribio la Bazoum kutoroka kutoka kizuizini

Nairobi – Viongozi wa kijeshi nchini Niger, wanasema wamezuia jaribio la aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohamed Bazoum, kutoroka kutoka kizuizini.

Msemaji wa uongozi huo wa kijeshi Amadou Abdramane amesema, jaribio la Bazoum , kutoroka lilitokea siku ya Alhamisi lakini likazuiwa
Msemaji wa uongozi huo wa kijeshi Amadou Abdramane amesema, jaribio la Bazoum , kutoroka lilitokea siku ya Alhamisi lakini likazuiwa AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa uongozi huo wa kijeshi Amadou Abdramane amesema, jaribio la Bazoum , kutoroka lilitokea siku ya Alhamisi lakini likazuiwa.Abdramane, amesema Bazoum aliyeondolewa madarakani mwezi Julai, pamoja na família yake, wapishi wake wawili na maafisa wa usalama wanaomlinda walijaribu kutoroka saa tisa usiku, lakini wakakamatwa.

Mohamed Bazoum alikuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa na harakati zake katika ukanda wa Sahel
Mohamed Bazoum alikuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa na harakati zake katika ukanda wa Sahel AFP - ISSOUF SANOGO

Aidha, jeshi linasema Bazoum akiwa na mke wake Haziza na mtoto wake wa kiume Salem, walikuwa wamepanga kutorokea nchini Nigeria, kwa usaidizi wa usafiri wa helikopta kutoka nchi ya kigeni.

Uongozi wa kijeshi unasema, umeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo lilitokea jijini Niamey lakini haujaeleza anakozuiwa Bazoum kwa sasa.

Jumuiya ya ECOWAS imekuwa ikitoa wito kwa kuachiwa huru kwa aliyekuwa rais wa Niger Mohammed Bazoum
Jumuiya ya ECOWAS imekuwa ikitoa wito kwa kuachiwa huru kwa aliyekuwa rais wa Niger Mohammed Bazoum AFP - KOLA SULAIMON

Mwezi Septemba; Mawakili wa rais huyo wa zamani walikwenda kwenye Mahakama ya Jumuiya ya ECOWAS kulalamikia kuzuiwa kwake, wakati huu Jumuiya ya Kimataifa ikishinikiza kuchiwa huru kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.