Pata taarifa kuu

Niger: Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa umewasili Chad

Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa wanaondoka nchini Niger, umewasili nchini Chad, jeshi la Ufaransa limethibitisha.

Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa wanaondoka nchini Niger, umewasili nchini Chad
Msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa wanaondoka nchini Niger, umewasili nchini Chad AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kanali Pierre Gaudilliere, msafara huo umewasili katika mji mkuu wa Chad N’Djamena baada ya siku tisa ukiwa barabarani.

Wanajeshi hao wanatarajiwa kuondoka tena nchini Chad wakielekea nchini Ufransa kwa kutumia usafiri wa angani.

Ufaransa iliaanza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger baada ya mapinduzi ya mwezi Julai
Ufaransa iliaanza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger baada ya mapinduzi ya mwezi Julai © THOMAS COEX / AFP

Kwa mujibu wa Gaudilliere, safari hiyo ya njia ya barabarani ilikuwa imefanikishwa kwa usaidizi wa wanajeshi wa Niger.

Ufaransa ilianza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger wiki iliyopita baada ya kuangushwa kwa utawala wa rais Mohamed Bazoum mwezi Julai, kiongozi huyo alikuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa na mikakati yake katika ukanda wa Sahel.

Mohamed Bazoum alikuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa na harakati zake katika ukanda wa Sahel
Mohamed Bazoum alikuwa mshirika wa karibu wa Ufaransa na harakati zake katika ukanda wa Sahel AFP - ISSOUF SANOGO

Karibia wanajeshi wa 1,400 wa Ufaransa walikuwa jijini Niamey na eneo la Magharibi mwa Niger katika juhudi za kupambana na makundi ya kijihadi ambapo walikuwa wakitumia silaha za kisasa ikiwemo ndege za kivita, helikopta na magari ya kivita pamoja na sila nyengine.

 

Msafara huo umewasili nchini Chad kwa kutumia usafiri wa barabara ambapo wamesafiri zaidi ya kilomita 1,600 wakisindikizwa na wenzao wa Niger.

Hatua ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger imekuja baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi
Hatua ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger imekuja baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi AP - Sam Mednick

Mji mkuu wa Chad N'Djamena ni makao makuu ya wanajeshi wa Ufaransa katika eneo pana la Sahel, karibia wanajeshi elfu moja wakiwa huko.

Jumatano ya wiki hii, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikuwa mwenyeji wa rais wa Chad Mahamat Idriss Deby kwa mazungumzo katika Ikulu ya Elysee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.