Pata taarifa kuu

Kiongozi wa Chad Mahamat Idriss anazuru Ufaransa

Nairobi – Kiongozi wa serikali ya mpito  nchini Chad Mahamat Idriss yuko nchini Ufaransa, ziara inayolenga kuimarisha uhusiano na kati ya nchi hizo mbili mbali na kutaka kufadhiliwa kumaliza kipindi cha mpito.

Derby pia analenga kuomba msaada kutoka kwa ufaransa kusadidi nchi yake kuwakabili idadi kubwa ya wakimbizi wanaotoroka vita kutoka taifa jirani la Sudan
Derby pia analenga kuomba msaada kutoka kwa ufaransa kusadidi nchi yake kuwakabili idadi kubwa ya wakimbizi wanaotoroka vita kutoka taifa jirani la Sudan AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Derby ambaye tayari amekutana na mwenyeji wake Emmanuel Macron jamatano, analenga kushawishi Ufaransa kuendelea kusaidia nchi yake kukabili makundi ya wanajihadi, na ufadhili wa kuanda kura ya maoni kuhusu katika mpya nchi hiyo mwezi disemba kuelekea kukamilika kwa kipindi cha mpito. 

Taarifa kutoka afisi ya rais Chad, imesema Derby, analenga kuheshimu makubaliano ya kumalizika kwa kipindi cha mpito mwaka ujao baada ya kura ya maoni baadaye mwaka huu, wakati huu ufaransa ikiendelea kuunga mkono utawala wake wa kijeshi. 

Kiongozi huyo wa Chad pia analenga kushawishi Ufaransa kuendelea kusaidia nchi yake kukabili makundi ya wanajihadi
Kiongozi huyo wa Chad pia analenga kushawishi Ufaransa kuendelea kusaidia nchi yake kukabili makundi ya wanajihadi AFP - LUDOVIC MARIN

Derby pia analenga kuomba msaada kutoka kwa ufaransa kusadidi nchi yake kuwakabili idadi kubwa ya wakimbizi wanaotoroka vita kutoka taifa jirani la Sudan. 

Ufaransa na Chad zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa muda, licha ya kwamba Chad inalenga kuanza kujitengemea hasa kiuchumi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.