Mamlaka ya Niger imeanza kuwageukia washirika wapya baada ya mapinduzi
Nairobi – Miezi miwili na nusu baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger mnamo Julai 26, dhidi ya Rais Mohamed Bazoum, nchi hiyo sasa imeanza kugeukia washirika wapya, baada ya kukabiliwa na vikwazo vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, Ecowas.
Imechapishwa:
Cheza - 01:09
Utawala wa kijeshi jijini Niamey umesema licha ya kukatiwa misaada ya kibinadamu, ya kifedha kutoka taasisi mbali mbali za kimataifa, na kusitishwa kwa ushirikiano na mataifa ya magharibi miongoni mwao Ufaransa, lakini pia Marekani, na Umoja wa Mataifa, lakini bado kuna uwezekano wa kuwapata washirika wapya, Taarifa ya ikulu ya rais jijini Niamey imesema.
Wadadisi wa mambo wanasema tukio la hivi punde la kumfukuza mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Niger Luiza Aubin, kuondolewa kwa wanajeshi wa Ufaransa, na kusitishwa kwa baadhi ya ufadhili wa kimataifa huenda yakachangia kwa nchi hiyo kutumbukia katika lindi refu la umasikini.
Utawala wa kijeshi nchini Niger umeshutumu kile unachokiita ujanja" unaofanywa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, chini ya ushawishi wa Ufaransa", ili kuidhuru nchi yao.
Siku ya Jumanne, Marekani ilitangaza kuondoa msaada wa kiasi cha dola milioni 500 ili kufadhili miradi ya maendeleo, Hali ambayo huenda ikaathiri pakubwa juhudi za maendeleo ya kiuchumi ya nchi hiyo.